Tiketi za elektroniki zitaanza
kutumika katika mzunguko wa nne wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakaoanza
Septemba 18 mwaka huu. Tayari benki ya CRDB ambayo ndiyo ilishinda tenda
hiyo imeshakamilisha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya matumizi ya tiketi
hizo katika viwanja vyote. (HM)
Hivi sasa Serikali ambayo ndiyo
inamiliki Uwanja wa Taifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
pamoja na CRDB zinashughulikia mfumo wa tiketi hizo kwenye uwanja huo
ambao ndiyo ulikuwa haujakamilika kwa matumizi katika upande huo.
Mfumo (system) iliyoko kwenye uwanja
huo inapishana na ule utakaotumiwa na CRDB, hivyo pande husika
zinashughulikia suala hilo ili mifumo hiyo iweze kuingilia.
Pia mashine za kuchapia (printer) kwa
ajili ya tiketi ambazo CRDB wameziagiza kutoka nje ya nchi zinatarajiwa
kuwasili mwishoni mwa mwezi huu.
Hivi sasa CRDB inashughulikia ufungaji
wa vifaa vya matumizi ya tiketi za elektroniki iwemo turnstiles kwenye
Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ambao mwanzoni hakuwemo kwenye mpango huo
kutokana na Mkoa wa Tabora kutokuwa na timu ya Ligi Kuu.
RATIBA YA LIGI WIKIENDI HII
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi kesho (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja saba tofauti huku mabingwa watetezi Yanga wakianza kutetea ubingwa wao kwa kuikaribisha Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi kesho (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja saba tofauti huku mabingwa watetezi Yanga wakianza kutetea ubingwa wao kwa kuikaribisha Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Uwanja wa Manungu ulioko Turiani
mkoani Morogoro utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam ya Dar es Salaam
na wenyeji Mtibwa Sugar. Oljoro JKT itaikaribisha Coastal Union kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Mgambo Shooting itaoneshana kazi na
JKT Ruvu ambayo hivi sasa iko chini ya Kocha Mbwana Makata. Mechi hiyo
itachezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Rhino Rangers itakwaruzana
na Simba katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mbeya City iliyopanda VPL msimu huu
itapimana ubavu na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya huku Ruvu Shooting ikiialika Mabatini, Mlandizi timu ya
Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Mzunguko wa pili wa ligi hiyo
utachezwa Agosti 28 mwaka huu. Baada ya hapo ligi itasimama kupitisha
mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Gambia na Tanzania (Taifa
Stars) itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul. VPL itaingia
mzunguko wa tatu Septemba 14 mwaka huu. Chanzo: tff
No comments:
Post a Comment