skills za kitaa

Sunday, August 11, 2013

Shilole sikuzina hesabika kuhusu (Colabo) lake na J - Lo


MSANII nyota kwenye tasnia ya filamu
na muziki Zuwena Mohamed 'Shilole'
baada ya kusemwa sana kutoweza kufanya (colabo) na msanii nguli wa Marekani
Jenifer Lopez 'J LO' sasa afunguka kurudi
tena kutimiza adhima yake.


Akizungumza Dar es Salaam Shilole alisema kuwa  baa ya shoo za fieta zinazotarajia
kuanza kwa  mwaka huu mapema hivikaribuni ataondoka kurudi Marekani kufanya
ngoma matata sana na mkali hiyo.

"Watu wanasema sana kuhusu mimi , mara Shilole hivi mara vile sasa wasubiri ngoma
nitakayofanya mimi na J- Lo mwaka huu huu lazima wafunge midomo yao,"alisema Shilole.

kuna habari ambazo zilijili kipindi Shilole aliporudi na kutangaza ujio wa (Colabo)
hiyo na gafla alijitokeza nyota wa zamani wa maigizo nchini akitokea Kaole ambaye kwa
sasa ni mtangazaji wa DTV Christina John 'Sintah'na kusema Shilole anaota ndoto
za mchana za kufanya (Colabo) na msanii huyo.

Nyota huyo alisema kuwa licha ya kurudi tena Marekani lakini
anaziara ya kwenda kutembelea nchini nne zingine za barani Ulaya.

No comments: