skills za kitaa

Sunday, August 18, 2013

Mkali wa Sinema za mapigano nchini Jimmy Master kutua na Double J Final


MSANII nguli katika anga za tasnia ya filamu nchini Jimmy Mponda
a.k.a  Jimmy Master baada ya  mashabiki wake kuwa wanamuuliza
kuhusu muendelezo wa sinema ya Double J iliyotoka katika
mfurulizo wa kwanza na wapili jamaa amefunguka kuwa
kutua na ujio wa Doble J Final.


Nyota huyo ambaye sinema zake zimeonekana kuwa na mapigano ya
kutisha amefunguka kuwa kama kawaida yake yamo matukio yanayoambatana
na matukio sahihi ya kipelelezi yanayovutia wadau kupatwa na hisia mara tu
watakapoiona filamu hiyo.




"Wadau wengi walikuwa wakiniuliza muendelezo wa sinema hii,
napenda kuwatangazia kuwa siku si nyingi wataanza
kuipata sinema hii,"alifunguka J Plus.

Ndani ya ujio huo jamaa amemshirikisha mbambe mwingine wa filamu
za mapigano Ibrahim Mbwana 'Bad Boy' pamoja na nyota kadhaa
kama Charles Magari pamoja na Hashim Kambi na Veronica Viankero, kwa habari kuhusu ujio huo pia tembelea www.mzimunitheatrearts.blogspot.com.

No comments: