Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe
pamoja na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo
muhimu ya kufanyiwa marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya
“Foolish Age” katika Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi.
Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni ya Proin Promotions ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi. Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya Foolish age ya msanii wa kike mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo nje ya maadili ya Kitanzania katika filamu hiyo....
Filamu hiyo ambayo
ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa Mlimani City
inahitaji marekebisho.
Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumiwa na waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni, Kwa mujibu wa Lulu Michael, juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda na ratiba kama ilivyopangwa.

No comments:
Post a Comment