skills za kitaa

Friday, February 22, 2013

DIAMOND AFUNGUKA NA KUJIFAGILIA



NGULI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Diamond' amesema, anajivunia kuweka historia ya kufanya onyesho, ambalo mashabiki wamelipa kiingilio kikubwa ili kumshuhudia.

Diamond ameeleza kupitia mtandao wake kuwa, katika maisha yake, hajawahi kufanya onyesho, ambalo mashabiki walilipa zaidi ya sh. 20,000.

Katika onyesho hilo lililofanyika wiki iliyopita kwenye ukumbi wa klabu ya Safari Carnival mjini Arusha, kiingilio kilikuwa sh. 150,000 kwa mtu mmoja.

"Kiukweli namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuweza kufanikisha onyesho hilo,"alisema msanii huyo, ambaye amewahi kushinda tuzo kadhaa za muziki za Kilimanjaro.

"Huwezi kuamini, licha ya kiingilio kuwa kikubwa, mashabiki walifurika pasipo hata mimi kutegemea. Kiukweli, ilinifariji sana,"aliongeza.

Kwa mujibu wa Diamond, wingi wa mashabiki hao ulidhihirisha kwamba watanzania wanathamini na kujali vipaji vya wasanii wao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

"Zamani shoo ya kiingilio kikubwa ilikuwa mpaka msanii atoke nje ya nchi. Hali hii inanipa changamoto ya kuzidi kufanya vizuri, kujituma na kuwa mbunifu zaidi,"alisema.

Diamond alisema moja ya mipango yake ya baadaye kimuziki ni kuitangaza Tanzania kimataifa.

Aliushukuru uongozi wa Safari Carnival na mashabiki wote wa muziki wa Arusha waliojitokeza kushuhudia onyesho hilo.

TYSON AK SHOW LOVE NA EVANDER HOLYFIELD




CHICAGO, Marekani

  Mike Tyson na Evander Holyfield walipokutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16.

Safari hii hawakukutana kwenye ulingo wa ndondi. Walikutana katika uzinduzi wa kinywaji kipya uliofanywa na Holyfield katika grosari ya Jewel-Osco iliyopo mjini Chicago.

Kabla ya tukio hilo, Tyson (46) alimwendea Holyfield (50) kwa furaha na kumkumbatia. Ilikuwa kama vile marafiki waliopoteana zamani wanafurahia kukutana.

Muda wote wa tukio hilo, Tyson alionekana akitabasamu kwa furaha na kuonyesha meno 32 nje wakati Holyfield akitoa kicheko tuuuuuu.

Diamond Platnumz having Dinner with Vj Penny


 
No comments:

Thursday, February 21, 2013

Goldie Hervey Ft, AY


Chokoraa

MWANAMUZI wa bendi ya muziki wa dansi nchini Khalid Chokoraa amesema akiwa ni
moja wa viongozi wa bendi ya Mapacha Watatu  ameibuka na kumkoromea kiongozio wa bendi mpya
ya muziki huo Mwinjuma Muumin anayeongoza bendiya  Victoria Sound.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Chokoraa amemkoromea Muumin kwa kusema kuwa nyota huyo
amefilisika kimuziki. 



"kitendo chake cha kuujibu wimbo wa 'Shamba la Twanga'
ni ushahidi kuwa enzi zake zimekwisha,"alisema Chokoraa.

Aliendelea kufunguka Chokoraa kwa kutamba kuwa  bendi ya  Twanga kupitia kwa uongozi wa Asha Baraka imwachie yeye kazi ya kumjibu Muumin.

Nyota huyo alienda mbali zaidi na kusema  "hakika kitu alichokifanya Muumin bendi
ya Twanga iniachie mimi kumjibu kwanza mimi na yeye tunatoka sehemu moja Bagamoyo hivyo
awezi kunishinda ."


Tayari bendi ya  'Mapacha Watatu'kwa sasa inajiandaa kwa ajili ya uzinduzi wa albamu mpya itakayozinduliwa mach 2 mwaka huu kwenye ukumbi wa Business Park maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaa.
Johmakini

Belle9:Afande Sele anafaa kuwa mbunge





MSANII nyota katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Belle9 amefunguka na kusema msanii nguli katika muziki wa Hip Hip nchini Afande Sele  anafaa kuwa mbunge 2015.

Nyota huyo  aliyabainisha hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Afande Sele amabaye tayari katangaza nia yake
ya kugombea katika Jimbo la Moroogoro Mjini
ifikapo mwaka 2015 amejikuta kupewa ufagio hilo na msanii Belle9.

"Ni mtu muhimu katika nafasi ya kuongoza jimbo
jamii kubwa huwa inamkubali  anastahili
kugombea jimbo hilo,"alisema msanii huyo.

Belle9 pia alisema anawazimia pia baadhi ya wasanii wengine waliowahi kubamba na nyimbo zao kusumbua anga za muziki.

Pia msanii huyo alisema amejipanga  kufikisha muziki kwenye 'levo' za kimataifa mwaka huu ambapo nchini Uganda yuko mbio kumshirikisha katika kazi zake za sanaa msanii Bebe Cool .

Muziki wa dansi





 Ukitaka kuongea muziki wa dansi uliingiaje nchini ni muhimu kujua historia ya mji wa Tanga. Wadau wanasema mji wa Tanga ndipo muziki wa dansi ulipoingilia nchini.

Wajerumani waliusambaratisha mji wa Tanga kwa
mizinga kati mwaka 1888 na 1889. Na baada ya hapo
kuujenga upya kwa kufuata mpangilio uliosababisha
Tanga kuwa na mitaa maarufu kama barabara ya kwanza
ya pili na kuendelea.

Wajerumani walianzisha shule ya kwanza ya serikali
Tanga 1892 na hapohapo wakanzisha bendi ya shule ya
kwanza, pamoja na kuwa Wajerumani hawakutawala muda
mrefu baada ya hapo lakini Waingereza waliiendeleza
sana bendi hiyo iliyokuwa ikipiga aina mbalimbali za
muziki wa kigeni.

Dansi ilianza kwanza kama klabu ambapo watu
walialikana kuja kucheza aina mbalimbali za muziki wa
kizungu mtindo maarufu unaojulikana kama 'ballroom
dancing'.

Aina hizi za klabu zilianzia Mombasa na
kuingia nchini kupitia Tanga na kisha kuletwa Dar es
Salaam na klabu iliyokuwa maarufu Tanga ili kujulikana
kwa jina  Tanga Young Comrades Club, klabu nyingine
ilianzishwa ikaitwa New Generation Club ambayo
ilianzisha matawi miji mbalimbali.



Wadau  wa elimu waliupoteza muziki, kwa miaka
ya nyuma katika kila shule kulikuwa kunafundishwa
somo la muziki lakini kwa kadri siku zinavyoenda
somo hilo linaonekana kupotea.

Msanii nguli katika muziki wa dansi nchini
John Kitime anasema kuwa takriba kila shule
ya sekondari miaka ya nyuma kulikuwa na kipindi
cha muziki ambapo mwanafundi aliweza kujifunza
muziki.

"Tulukuwa na aina za muziki , tulitumia sana
muziki wa Afro na wanafunzi katika kipindi hicho
cha miaka ya nyuma aliweza kuchagua aina ya sanaa.

"Wapo wanafunzi wengine walipendelea kujifunza
muziki wa asili tu , nao walikuwa na nafasi yao,
kwa kweli kila sanaa ilifundishwa katika kipindi
cha muziki shuleni,"anasema Kitime.

"Tulikuwa tukikutana na shule zingine katika masuala
ya kupiga muziki ali iliyochochea mafanikio ya
wanamuziki wa dansi kupatikana nchini tofauti na
sasa."

Kitime ambaye ni mdau katika medani ya
muziki nchini anasema kuwa kutokana na mambo
yanavyokwenda kwa hivi sasa katika taswira ya sasa
katika muziki wa sasa ambao ni Bongoflava.

Kitime anapasua jambo kwa kusema kuwa hali ya
kutofundishwa masomo ya muziki kama yaliyokuwepo
awali ndio haswa mpasuko katika muziki.

"Bendi nyingi za dansi zilizowai kuwika wanamuziki
wengi walianzia kuwika na kuonekana vipaji vyao
wakiwa bado shuleni sehemu waliyo pata kufundishwa
masomo ya muziki.

"Kwa sasa Tanzania haijulikani inafanya muziki wa
aina gani kwani  hatuna tena asili ya muziki wa

Tanzania kama ilivyo wai kuwepo,   wanamuziki wengi
walipata kutia heshima katika anga za muziki miaka ya

nyuma.

Kuhusu yeye kushauri vijana wa muziki wa Bongoflava
anasema awezi kushauri kitu chochote katika muziki
huo kwa sababu yeye ajapata kuujua maka sasa
aufahamu.

"Siwezi nikashauri kituambacho mimi sikijui ,
mie siujui muziki huo na sijawai kufanya muziki
wa aina hiyo , sasa siwezi kushauri chochote,
mtu anashauri kituanacho kifahamu,"anasema Kitime.

Kitime anasema kuhusu kelele za wasanii kuibiwa
kazi zao wasanii nyota huyo mkongwe katika anga za
muziki wa dansi ana tiririka kwa kusema kuwa.

"Wadau wa muziki wanakuwa wanailaumu serikali ,
kuwa wanaibiwa kazi zao za muziki lakini wao
wanawajua wezi wao , kimusingi anatakiwa alaumiwe
anayemjua mwizi .


"Na si serikali kwani vyombo vya sheria vipo
mtu anatakiwa akamate mwizi na kumpeleka
katika vyombo husika na kitendo cha  kulalamika tu

mdomoni na kusema serikali haiwajali, na wakati wao
wanamjua mwizi wao aitoshi kumkataza mwizi asiibe."

Kitime anapasua tena jibu kwa kusema kuwa yeye
ametoka katika familia ya muziki kwani mama na baba
yake ni wazazi ambao waliopata kufahamika katika
tasnia ya muziki hivyo hali hiyo ilimfanya yeye
kuchochea nyota yake kunga'ra katika tasnia ya muziki
wake.

Pia John Kitime ni mtu ambaye hachoki kuhifadhi na
kusambaza historia ya muziki nchini Tanzania kuanzia
ule tuliouita 'Muziki wa Dansi' .

Kitime anafanya hivyo kwa kutambua kwamba endapo
juhudi binafsi hazitofanywa,basi kizazi cha Tanzania
cha miaka kumi ijayo,hakitojua wapi tulitoka katika
medani za muziki.

Wataanzia tulipo na pengine kuishia tulipo.Wadau
kadhaa wameisha wai  kumuomba Kitime asisahau
kuandika kitabu ili kuhifadhi vizuri zaidi historia
muhimu.Kwani kitime hadi sasa ni mdau wa ulimwengu
wa sasa anaye elimisha jamii kupitia mitandao
ya kijamii anamiliki Blog tano za kijamii.Inatoka gazeti la Majira.