skills za kitaa

Sunday, October 12, 2014

Nakaaya atua na albamu mpya



Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing 
Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing MSANII wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari hivi karibuni alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa kuzindua albam mpya iendayo kwa jina la Blessing yenye nyimbo kumi na mbili (12). Albam hiyo ambayo ni albam yake ya pili ilizinduliwa jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashabiki wa muziki wake kutoka mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro. 

Huku akiungwa mkono na wasanii wenzake kutoka hapa hapa nchini na nje ya nchi. Uzinduzi huo ulipambwa na burudani kabambe kutoka kwa Hisia, G Nako, Jambo squad wote kutoka Arusha, Naaziz kutoka Kenya, na Nakaaya mwenyewe yote hiyo nikumpasapoti msanii mwanzao. Akizungumza kwa furaha mwanadada Nakaaya Sumari alisema kuwa anawashukuru sana wote waliokuja kumuunga mkono katika uzinduzi wake. “Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kunipa sapoti ya nguvu kwani wa lijitokeza kwa wingi, nimefurahi sana kwani huu ni mwanzo mzuri,” alisema Nakaaya.
 “Albam hii imebebwa na wimbo wa Blessing ambao ni maalum kwa mwanangu kipenzi kwani yeye ni Baraka kwangu hata napokua mbali naye bado nakua na matumaini na faraja,” Nakaaya aliongeza kwa msisitizo. Albam ya Blessing ipo sokoni sasa na inanyimbo nzuri za kuelimisha, kuburudisha na kuliwaza kama vile Utu uzima dawa, Temana na watu, Blessing, Beautiful, I am an African, Sister sister, Ngufurie, na Mwanamke shujaa, kubwa ni kumpa sapoti kwa kununua albam hii.

Friday, October 3, 2014

Said Fella aelezea jinsi alivyosaka mchongo wa Shaa kulipwa kupitia YouTube


 Video: Said Fella aelezea jinsi alivyosaka mchongo wa Shaa kulipwa kupitia YouTube
Meneja mkongwe na muewezeshaji wa Mkubwa na Wanae, Said Fella amefunguka kuhusu njia alizotumia kutafuta nafasi ya biashara ya wasanii wake akiwemo ‘Shaa’ kulipwa pale kazi zake zinapowekwa YouTube.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Fella amesema yeye na Babu Tale waliumiza kichwa baada ya kuona wasanii wa Kenya wanaingiza pesa hata kama hawajatoa wimbo mpya, bila kutegemea shows na ndipo walipoamua kusafiri hadi Nairobi kuhakikisha wanafahamu nini hasa cha kufanya.
“Kweli tukaenda Kenya, tukaenda kukutana watu tukawauliza ‘jamani nyie mnaendaje mbona sisi tukiwapelekea wenzetu wanaotuuzia ringtone hapa Tanzania hatupati faida ile’. Lakini unakuta Jua Cali au Nyota Ndogo kafanya muziki zamani lakini anaendelea kula faida.” Amesema Said Fella.
“Yaani tumesafiria tobo na ndio maana tumelipata tobo. Hata juzi kati Babu Tale na Diamond walivyoenda Nigeria kwenda kusaka tobo…na ndio maana tunasema timu yetu Saka Tobo ili kwenda kuangalia wenzetu wanafanya nini na tunakwenda wapi. Kwa hiyo huwezi kumfuata tu mtu ukamwambia ebwana tobo hili…wajetuwaoneshe. Watanzania tunapendana.” Said Fella ameiambia tovuti ya Times Fm.
Shaa ambaye kimuziki anasimamiwa na Said Fella hivi sasa analipwa kwa kazi anazoweka kwenye channel ya YouTube.
Video yake ‘Sugua Gaga’ imevunja rekodi ya video za bongo flava kwa kuangaliwa zaidi YouTube, hadi leo imeangaliwa zaidi ya mara 4,656,000.

NIGHT OF CELEBRITIES