Actress maarufu nchini Irene Paul anadaiwa kuwa mjamzito lakini mwenyewe anadaiwa kuficha watu wakiwemo mapaparazi ili wasijue kuwa tayari kanasa. Inadaiwa star huyo anayetamba na filamu kibao ana dalili zote za ujauzito kwa mujibu wa chanzo kimoja kilicho karibu nae lakini haijulikani kwanini hataki kuweka wazi hata kwa watu wake wa karibu. "sijajua kwanini hataki watu wajue kama ana ujauzito labda anataka watu washtukie tu amejifungua mtoto. Lakini ajue yeye ni star hata afanyeje hawezi kulificha tumbo lake litakapokuwa kubwa" kilisema chanzo hicho kikizungumza na mtandao mmoja.
Baada ya kupata habari hizo ilibidi Swahiliworldplanet imtafute Irene Paul ili kusikia upande wake kama kweli ni mjamzito au lah lakini mpaka tunaandika habari hii muigizaji huyo hakutoa ushirikiano wowote ule.
Irene Paul
No comments:
Post a Comment