Familia ya wasanii wa kike wanaochana aka Femcees inazidi kuongezeka baada ya Flave Music Africa (FMA) kumleta kwenu msanii mpya kabisa ambaye pia ni Actress & Model, anaitwa Rukkii. Ni mtoto mmoja mzuriiii sana ambaye amekuja rasmi na ngoma mpya kabisa inayoitwa Mimi na Wewe.
Rukkii, msanii mpya wa Bongo flava
Kwenye wimbo huu, mrembo huyo (Rukkii) ameamua kumshirikisha msanii mkongwe wa muziki wa Dance ambaye ana asili ya DRC, Christian Bella. Huu ni wimbo mzuri sana, unaelezea mapenzi ya watu wawili walioshibana wakipeana ahadi za kutoachana. Rukkii raps nicely na Bella kwa upande wake wa chorus ameutendea haki.
No comments:
Post a Comment