skills za kitaa

Thursday, August 8, 2013

Cheki Jimmy Master na heka heka za ujio mpya wa Doble J Final






YULE muongozaji na mwigizaji Jimmy Mponda 'Jimmy Master' aliyetikisa
 na mfululizo wa filamu za misuko iliyotoka sehemu ya kwanza hadi ya
tatu na baadaye kujiongezea jina lingine akiitwa J Plus.

Kwa sasa nyota huyo amefunguka  kuwa yukombioni kutoa muvi ya mwisho
inayoitwa Doble J Final  huku ujio huo ukiwa ni wa mwisho kutoka baada
ya kutangulia  na Doble J sehemu ya kwanza na yapili zilizotoka mwaka jana.


"Mwaka jana nilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu hususani
 wanaopagawa na filamu za mapigano na kujawa mambo ya  kipelelezi,"alisema J Plus.

Alisema Doble J Final pia ni ujio wake wa filamu nyingine ya mapigano na
 kuna heka heka za kipelelezi ndani. J Plus aliyezoeleka sasa katika kuonesha
ubabe wa kufa mtu , kwa sasa ujio wake huo unao tazamiwa kuingia sokoni mapema tu ,
 mwezi ujao .

Pia Jimmy Master amemshirikisha mbabe mwingine katika filamu za mapigano Ibrahim Mbwana  'Bad Boy'
na pia wamo nyota wengine katika dulu la filamu kama Charles Magari , Hashim Kambi .

No comments: