skills za kitaa

Sunday, August 25, 2013

Matapeli waigusa ikulu



IKULU a4b39MTANDAO hatari wa matapeli unaotumia mbinu mbalimbali, ikiwemo za kujipachika vyeo vya maofisa usalama wa Taifa, sasa umefanikiwa kupenya na kuanza kutumia viunga vya Ikulu iliyopo Magogoni, Jijini Dar es Salaam, kufanikisha hujuma zao.
Taarifa zimethibitisha pasipo shaka kwamba Ikulu ya Jijini Dar es Salaam sasa inataka kugeuzwa kuwa kichaka na matapeli hao, ambao pia wamejivika undugu wa kifamilia na viongozi wakubwa nchini.
Mtandao huo, ambao unaaminika kuumiza watu mbalimbali, ukiwalenga zaidi akina mama na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, anayetumikia kufanikisha utapeli huo kupitia viunga vya Ikulu, ni mvulana anayejiita Baraka Tibaijuka.

No comments: