Ofisa Mkuu wa Biashara wa Zantel, Sajid Khan akimkabidhi jezi,
Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo kwa niaba ya klabu ya African Lyon
ya Dar es Salaam, katika hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro),
Dar es Salaam wakati wa kutangaza kuingia mkataba wa kudhamini klabu
hiyo kwa miaka mitatu. Wanaomfuatia Thadeo ni Meneja Mkuu wa African
Lyon, Rahim Kangezi ‘Zamunda’ na Charles Otieno, Mkurugenzi wa Ufundi wa
African Lyon. Kulia kabisa ni mchezaji chipukizi wa Lyon, Jarufu
Magesa, ambaye anapelekwa na klabu Marekani kusoma. Lyon itashuka
dimbani jioni hii kumenyana na Simba SC katika mchezo wa ufunguzi wa
Ligi Kuu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
CHANZO CHA HABARI: BIN ZUBEIRY
CHANZO CHA HABARI: BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment