Raia wa Somalia na viongozi wa kisiasa
walipokea kwa furaha matokeo ya uchaguzi wa Rais jijini Mogadishu
Jumatatu (tarehe 10 Septemba) ambayo yalileta ushindi wa mwanataaluma na
mwanaharakati wa jamii ya kiraia Hassan Sheikh Mohamud, kiongozi wa
chama cha Amani na Maendeleo.
Katika
hotuba yake ya kwanza kwa taifa , Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
alisema, "Sasa ni wakati wa mabadiliko nchini Somalia." [Mahmoud
Mohamed/Sabahi]
Mohamud alimshinda aliyekuwa
Rais wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho Sheikh Sharif Sheikh Ahmed
katika duru ya pili ya uchaguzi, 190 kwa 79.
Wachambuzi wameelezea uchaguzi
huu kuwa, wa kwanza wa aina yake nchini Somalia kwa zaidi ya miongo
miwili, kama ukamilishaji wa historia kwa Somalia na mwanzo wa mpito wa
nchi wa kuelekea kwenye demokrasia.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa
na profesa wa chuo kikuu Ahmed Moalim Ahmed alisema ushindi wa Mohamud
ni mwanzo wa hatua mpya katika mpito wa kisiasa wa Somalia.
"Tunatarajia kuwa hatua hii ya
kihistoria ya kuchagua rais mpya kwa nchi itaonyesha kipindi kipya cha
utulivu na mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe,"," Ahmed aliiambia
Sabahi. "Ushindi wa Hassan Sheikh Mohamud kama rais ni ishara kuwa
Somalia imeingia kwenye hatua mpya na kipindi cha wababe wa vita
kimekwisha."
"Tunatarajia kuwa hali katika
nchi itaboreka na kuwa kama Wasomalia tutaweza kuondoa matatizo yoyote
ambayo tumeyapitia kwa miaka iliyopita," alisema.
No comments:
Post a Comment