skills za kitaa

Wednesday, September 12, 2012

WEMA ALIZWA TENA


Musa Mateja, Dar es Salaam BEAUTIFUL Onyinye wa Bongo, Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alijikuta akipata wakati mgumu baada ya kukombwa vioo vya gari lake aina ya Toyota Mark X na vibaka wa Moshi, Kilimanjaro, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Chuo cha Ushirika ambapo staa huyo alikuwa amehudhuria uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Akiwa katika burudani hizo, Wema ambaye muda mwingi alionekana kuwa mtu mwenye furaha ghafla alibadilika na kuishiwa na furaha alipolikuta gari lake likiwa limekongolewa vioo vyote vya pembeni.


Gazeti hili lilizungumza na Wema kuhusu tukio hilo ambaye alionekana kushangazwa na tukio hilo na kusema kuwa hakutarajia kukutana nalo kwa kuwa alikuwa akiwaheshimu sana watu wa Moshi.
“Imeniuma sana baada ya kukuta gari langu limekongolewa, wameiba vioo na ukiangalia nipo ugenini, halafu magari ni mengi yaliyokuwa yamepaki uwanjani, kwa nini yasiibiwe hayo mengine wakaiba langu tu, dah! imenikera sana,” alisema Wema kwa uchungu.
Hilo ni tukio lingine la Wema kulizwa, alishawahi kuibiwa nyumbani Sinza jijini Dar baada ya wezi kuruka ukuta na kumkomba baadhi ya vitu vya thamani, pia alishawahi kuibiwa vitu vingine ndani ya gari Uwanja wa Taifa.Inatoka kwa mdau.

No comments: