skills za kitaa

Tuesday, September 4, 2012

UONGOZI WA CCM DMV YA SISITIZA KWA WANACHAMA WAKE KUHUDHURIA KWA WINGI KWENYE MKUTANO WA NSSF WESTADI



P.O.BOX 56356 WASHINGTON DC 20040
Email address:ccmwashdc@gmail.com

TAARIFA YA WANA CCM KUHUDHURIA MKUTANO WA JUMUIYA YA WATANZANIA- DMV

Uongozi wa chama cha Mapinduzi unatangazia wanachama wake wote wa CCM waishio maeneo ya DMV kuudhuria kwa wingi kwenye mkutano wa NSSF WESTADI siku ya September 5, 2012, ulioandaliwa na jumuiya ya watanzania hapa DMV.

Huu ni mkutano muhimu sana kwa sisi watanzania tunaoishi nje ya nchi na ni chimbuko la ufumbuzi wa tatizo la gharama za usafirishaji mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania.

NSSF WESTADI ni mpango wa bima ya ustawi kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi. Lengo kubwa la mpango huu wa bima:

1. Kufidia watanzania wote waishio nje ya Tanzania ikiwamo kuchagua wategemezi wanne wa kuwawekea bima kupitia faida ya Bima ya Afya ya jamii.

2. Endapo Mtanzania anayeishi nje ya nchi atatembelea nyumbani (Tanzania) basi mkewe au mwenyewe anafaidika na mpango huu wa bima pale atakapokuwa mgonjwa.

3. Endapo Mtanzania anayeishi nje ya Tanzania atafariki dunia basi NSSF WESTADI wataweza kufidia gharama za kusafirisha mwili wa marehemu, ticket ya msindikizaji wa mwili wa marehemu na utunzaji wa mwili wa marehemu.

Tafadhali tunawaomba wa CCM DMV tuunge mkono juhudi za viongozi wa jumuiya ya watanzania DMV za kuleta uongozi NSSF WESTADI hapa DMV . Tunatoa mwito kwa wana CCM kufika mapema siku hiyo na ili tuweze kufaidika na mpango huo wa bima.

Asanteni

Imetolewa na mwenyekiti wa Tawi DMV Loveness Mamuya

No comments: