The President extends his warmest wishes to all those celebrating the Jewish HIgh Holidays.
Ni katika shamba la Kapunga Rice Project.
Wazazi wacharuka na kuanza kujenga shule mpya mahali alipobomoa mwekezaji.
Zaidi ya shilingi milioni 2.5 zachangwa papo hapo.
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Wanafunzi 23 wa Shule ya Msingi
Kapunga,Kijiji cha Mapogolo,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamenusurika
kifo baada ya kula mikate inayosadikiwa kuwa na sumu mnamo mwishoni mwa
mwezi Agosti mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti
wa Kijiji hicho Bwana Ramadhani Nyoni na mzazi mmoja wapo wa watoto
waliokumbwa na janga hilo la kusikitisha na kuhatarisha uhai.
Mzazi huyo ambaye hakupenda jina
lake kutaja amesema yeye ilimlazimu kununua lita 20 za maziwa,kisha
kuwanywesha watoto hao na kuokoa maisha yao ambapo hali zao zimetajwa
kuendelea vema.
Wakazi wa kijiji hicho
wakionekana kukerwa na kitendo hicho iliwalazimu kuitisha mkutano wa
hadhara na kuazimia kujenga shule mpya ili kuwaondoa watoto katika shule
iliyopo katika shamba la mwekezaji.
Mbali ya wananchi kukerwa na
vitendo vya kikatili vya mwekezaji huyo,pia Walimu wamefurahia uamuzi wa
wanakijiji kuamua kujenga shule mpya katika himaya ya kijiji ili
kuondoa adha ya kutembea umbali wa kilometa 52 kwenda na kurudi kutoka
Chimala,ambako ndipo walipopanga kutokana na uhaba wa nyumba kijijini
hapo na zilizopo shambani kwa mwekezaji walimu hao hufukuzwa mara kwa
mara.
No comments:
Post a Comment