skills za kitaa

Wednesday, September 12, 2012

‘STEVE R&B’ AREJEA BONGO BAADA YA KUWA ULAYA KWA MIEZI SITA AKIFANYA SHOW…!!


MSANII Steve R&B ambaye alitamba na ngoma kibao ikiwemo ‘One Love’, aliyomshirikisha Baby Boy, sasa amefunguka na kuzungumza na mtandao wa DarTalk, kuwa kitu kilichomfanya kuwa kimya ni kutokana na safari ndefu aliyokuwa nayo ya kimuziki nchi za Ulaya iliyodumu kwa takribani miezi sita.

Steve alisema kuwa katika safari hiyo alifanya show katika nchi nyingi kama Germany, Italy, Australia na Swaziland, ambako kote alifanya makamuzi ya hatari kwa ajili ya katangaza jina lake pamoja na taifa lake kwa ujumla.

Hata hivyo alisema kuwa anaamini mashabiki wake watakuwa wamemisi vitu vyake, na katika hilo anadai kuwa sasa amekuja na staili mpya ujio kwa ajili ya kuonesha kile alikifanya nje kwa miezi hiyo sita.

Aliongeza kuwa baada ya kurudi kuna ngoma ambayo ameshaifanya na inakaribia kwenda sokoni ambayo inakwenda kwa jina la ‘Radio’ ambayo ndani yake anapatikana Ommy Dimpoz.

“Mashabiki wangu wanaweza kusema nilikuwa kimya sana, kama unavyojua kila mtu anazungumza analojua, lakini ukweli ni kwamba nilikuwa kimya kwa sababu nilikuwa Ulaya ambapo nilienda kwa ajili ya show,” alisema.Inatoka kwa mdau.

No comments: