Baadhi wa wanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta.
Bendi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta itakuwa na ziara ya maonyesho ya siku tatu katika mikoa ya Iringa na Mbeya. Siku ya kwanza Twanga Pepeta inataraji kufanya onyesho mkoani Iringa tarehe 14-09-2012 siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Highland. Kesho
yake siku ya Jumamosi tarehe 15-09-2012 watakuwa Jijini Mbeya ndani ya
City Pub na siku ya Jumapili tarehe 16-09-2012 watamalizia kufanya
ziara ya maonyesho katika ukumbi huo huo wa City Pub kwa kufanya
Bonanza maalum kwa ajili ya wakazi wa Jiji la Mbeya na maeneo ya jirani. Matayarisho
yote muhimu ya ziara hii ya maonyesho yamekamilika na Bendi inataraji
kuondoka mara baada ya kumalizika kwa onyesho la kila siku ya Alhamisi
tarehe 13-09-2012 linalofanyika Club Maisha Oysterbay. Bendi inataraji kurudi mara tu baada ya onyesho la mwisho litakalofanyika siku Jumapili tarehe 16-09-2012 Jijini Mbeya. Twanga
Pepeta itakapokuwa katika ziara, Itamtambulisha Mwimbaji wao mpya
Kalala Jr aliyerejea hivi karibuni kutoka katika Bendi ya Mapacha
Watatu. Sambamba na utambulisho huo pia itatambulisha nyimbo zao mpya
za “Ngumu Kumeza” ilyotungwa na Mirinda Nyeusi, “Nyumbani ni Nyumbani”
iliyotungwa na Kalala Jr, “Walimwengu” iliyotungwa na Jumanne Said na ”
Mapambano ya Kipato” iliyotungwa na Mwinjuma Muumini. Mara baada ya
kurejea Twanga Pepeta itaendelea kufanya maonyesho yake kama kawaida
Jijini Dar es salaam katika kumbi za Club Billicanas siku ya Jumatano,
New Club Maisha siku ya Alhamisi, Free Time Resort Ukonga Banana, Mango
Garden siku ya jumamosi na Jumapili mchana Leaders Club na usiku
Mzalendo Pub. MUDDY K EVENTS MANAGER TWANGA PEPETA. |
No comments:
Post a Comment