MABAO
yaloyofungwa na Emmanuel Okwi, Daniel Akuffour na nassoro Cholo jana
yaliwawezesha mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Simba
kuanza vyema kutetea taji lao baada ya kuibamiza African Lyon mabao 3-0
katika moja ya mechi za ufunguzi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Wakati Simba iliibuka na ushindi huo mnono wa
mabao, watani wao wa jadi Yanga walishindwa kufurukuta mbele ya Prisons
baada ya kulazimishwa kutoka nayo suluhu katika mechi iliyochezwa kwenye
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Okwi alikuwa wa kwanza
kuitungua Lyon baada ya kuingia na mpira ndani ya eneo la hatari la
Lyon, akawatoka mabeki wawili na kupiga shuti la mguu wa kushoto
lililotinga wavuni. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.
Akuffour
aliiongezea Simba bao la pili baada ya Okwi kuangushwa ndani ya eneo la
hatari wakati alipokuwa akienda kusalimiana na kipa Abdul Seif wa Lyon.
Bao la tatu lilifungwa na beki Cholo, kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Mrisho Ngasa, ambaye alikuwa nyota ya mchezo kwa Simba.
Lyon ilipata nafasi nzuri ya kufunga bao wakati ilipozawadiwa penalti kipindi cha kwanza, baada ya Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, lakini shuti la Sunday Bakari liligonga mwamba wa pembeni wa goli.
Lyon ilipata nafasi nzuri ya kufunga bao wakati ilipozawadiwa penalti kipindi cha kwanza, baada ya Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, lakini shuti la Sunday Bakari liligonga mwamba wa pembeni wa goli.
MATOKEO MECHI ZOTE LIGI KUU LEO
Simba 3-0 African Lyon
Kagera Sugar 0-1 Azam FC
Prisons 0-0 Yanga
Coastal Union 1-0 Mgambo JKT
Toto African 1-1 JKT Oljoro
Polisi Moro 0-0 Mtibwa Sugar
Simba 3-0 African Lyon
Kagera Sugar 0-1 Azam FC
Prisons 0-0 Yanga
Coastal Union 1-0 Mgambo JKT
Toto African 1-1 JKT Oljoro
Polisi Moro 0-0 Mtibwa Sugar
JKT Ruvu 2-1 Ruvu Shooting.Inatoka kwa mdau.
No comments:
Post a Comment