Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa CPA
Africa akitambulisha ujumbe wa Tanzania (hawapo pichani) na baadhi ya
Maafisa waliohuduria mkutano huo mjini Colombo Sri Lanka. Ujumbe wa
Tanzania unaongozwa na Mhe. Anne Makinda, Spika wa Bunge, Mhe. Zitto
Kabwe, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Hamad Rashid Mohamed, na Mhe.
Muhonga said Ruhwanya. Waliosima wa Kwanza kulia ni Ndg. Said Yakubu,
Afisa Dawati wa CPA Tawi la Tanzania na Kaimu Katibu wa CPA kanda ya
Afrika Ndg. Demitrius Mgalami.
Chama cha Mabunge
wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, (CPA Africa Region)
wamekutana kujadili mipango mbalimbali ya umoja wao katika Mkutano wa 58
wa CPA Dunia unaoendelea Mjini Colombo Sri Lanka. Pamoja na Mambo
mengine, Kanda hiyo ya Afrika imejadili namna ya kuimarisha chama hicho,
pamoja na maswala mbalimbali ya kiutendaji ndani ya Chama hicho ikiwa
ni pamoja na msimamo wa Afrika katika maswala kadhaa ndani ya chama
hicho duniani. |
No comments:
Post a Comment