Balozi
wa Marekani nchini Libya na wafanyakazi wengine wa ubalozi huo wameuawa
kutokana na mashambulizi ya roketi katika mji wa Benghazi
yanayohusishwa na maandamano ya Waislamu kupinga filamu inayomkashifu
Mtume wao.
Afisa mmoja wa serikali ya Libya
amethibitisha kwamba Balozi Chriss Stevens na wafanyakazi wengine
watatu wa ubalozi huo waliuawa kwa roketi lililorushwa kwenye gari ya
ubalozi. Hata hivyo, haikubainika mara moja kama balozi huyo alikuwamo
kwenye gari iliyoshambuliwa, au alikufa usiku wa kuamkia leo, baada ya
waandamanaji wenye silaha kuuvamia ubalozi huo mjini Benghazi.
Waandamanaji hao walikuwa
wamekasirishwa na filamu moja ya Hollywood ambayo inayakashifu kiongozi
wa Waislamu, Mtume Muhammad. Maandamano kama hayo pia yalifanyika mjini
Cairo, Misri, ambako maelfu ya waandamanaji waliuvamia ubalozi wa
Marekani, lakini bila kuwapo visa vya mashambulizi.
Wakristo wa madhehebu ya Koptik
nao wamekusudia kufanya maandamano kupinga filamu hiyo, wakisema kuwa ni
matusi kwa imani za watu wote.
Romney apata mwanya
Mgombea wa urais wa Marekani kwa
tiketi ya chama cha Republican, Mitt Romney, amelitumia tukio hilo
kuushambulia utawala wa Rais Obama kwa kuwa pamoja na waandamanaji wa
Kiislamu wenye siasa kali na sio pamoja na Wamarekani.
No comments:
Post a Comment