Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame MwadiniWatanzania
bara wanaoishi Zanzibar wataanza kusajiliwa na kupewa vitambulisho
maalum sawa na raia wa nje ya Tanzania wanaoishi Zanzibar.
Kwa
Mujibu wa muswada wa marekebisho ya sheria ya Usajili ya Mzanzibari
mkaazi namba 7 ya mwaka 2005 kazi ya kuwasajili itaanza kufanyika miezi
mitatu baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.
Muswada huo
unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini,
Oktoba 10 mwaka huu.
Kifungu cha 6A (1) cha muswada kimeleza
kwamba kila mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kujisajili katika Ofisi
ya usajili wa vitambilisho vya Mzanzibari mkazi.
Muswada huo umeleza kwamba zoezi hilo pia litawagusa raia wa kigeni ambao wanaishi Zanzibar na kufanya kazi au biashara.
Kifungu
cha 6A (3) kimeleza aina ya wageni wanaotakiwa kusajili kwa mujibu wa
sheria hiyo wanaofanyakzi Zanzibar ama kwenye taasisi ya umma au binafsi
pamoja na wanaofanyabiashara visiwani humo.
“Muajiri wa mkazi
asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kutoa taarifa za mtu huyo kwa mkurugenzi
au afisa msajili ndani ya siku 60 kuanzia ajira yake au ikiwa ameajiriwa
kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii,” umesisitiza muswada huo.
Aidha,
muswada huo umefuta kifungu cha 7 na watu wote watakaosajiliwa
watatakiwa kuchukuliwa alama za vidole badala ya kidole gumba kimoja kwa
mujibu wa sheria hiyo.
Akizungumza na NIPASHE Mkurugenzi wa
usajili wa Vitambulisho vya Uzanzibari mkazi Mohamed Juma Ame, alisema
serikali imeamua kuwasajili watu hao baada ya kubainika kuwepo watu
wanaopewa vitambulisho hivyo kinyemela.
Alisema kwamba hali hiyo
imekuwa ikifanyika baada ya vitambulisho hivyo kuonekana kuwa ni nyenzo
muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika upatikanaji wa huduma za
jamii.
Mohamed alisema sheria hiyo pia itasadia kuwatambua watu
wanaoingia na kutoka Zanzibar maeneo wanayoushi na kazi wanazofanya
Zanzibar.
Hivi karibuni Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi Zanzibar wameshindwa
kunufaika na ajira katika sekta ya Utalii kutokana na kazi hizo
kuvamiwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar ikiwemo Tanzania bara. SOURCE:IPPMEDIA |
No comments:
Post a Comment