skills za kitaa

Sunday, September 16, 2012

PIGO MAN UTD, ROBIN VAN PERSIE AUMIA VIBAYA


LONDON, England
MANCHESTER United huenda ikapata pigo lingine la majeruhi, baada ya mshambuliaji wake nyota, Robin Van Persie kuumia vibaya katika mchezo wa kimataifa wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia za 2014.
Van Persie aliumia katika mchezo, ambao Uholanzi ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Hungary. Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal aliyejiunga na Manchester United majira ya kiangazi, anadaiwa kuumia vibaya mguu wake wa kulia.
Kocha Mkuu wa Uholanzi, Louis van Gaal alimtoa mshambuliaji huyo baada ya kuumia. Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema ana hofu kubwa ya kumkosa Van Persie katika baadhi ya mechi kutokana na kuumia vibaya.
Kuumia kwake ni pigo kubwa kwa Manchester United kwa vile tayari timu hiyo imemkosa mshambuliaji nguli Wayne Rooney, ambaye atakuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa mwezi huu baada ya kuchanika paja.
Van Persie (29) tayari ameifungia Manchester United mabao manne katika mechi tatu alizocheza. Pia aliifungia Uholanzi mabao mawili iliposhinda Uturuki mabao 2-0 Ijumaa iliyopita.
Katika mchezo mwingine, Ujerumani ilishinda mabao 2-1 ilipovaana na Austria. Mabao ya Ujerumani yalifungwa na Marco Reus na Mesut Ozil, aliyefunga kwa mkwaju wa penalti.
Nayo Ufaransa ilivuna mabao matatu dhidi ya Belarus katika mchezo wa kundi I, ikiwa ni mwanzo mzuri kwa kocha mpya Didier Deschamps.
Sweden ilishinda mabao 2-0 ilipovaana na Kazakhstan wakati mabingwa wa zamani wa Kombe la Dunia, Italia walishinda bao 1-0 katika mchezo wao dhidi ya Malta.

R.I.P. Tupac Shakur: Heaven Has a Ghetto

by Jake Crates

Tupac Shakur
Today (September 13), Hip-Hop fans across the globe bow their heads in remembrance of one of Hip-Hop’s most prolific icons. Gone but surely not forgotten, fans are likely playing Tupac’s music across the globe from Africa to Europe, from South Central L.A. to the Bay, from Brooklyn to Baltimore. From his humble beginnings as the son of a Black Panther engaged in the arts, to his final days at Death Row amidst a swirl of negative media attention and governmental pressure, Tupac aspired to be impactful and influential to our urban communities.
To this day, the Thug Life brand is etched in Hip-Hop history like words etched in stone, as rappers, fans and loved ones will never forget the passion, enthusiasm, and care that ‘Pac put into his rhymes and his music for ghettos across the globe. Tupac’s fans were of all races, faces, and places, but he was especially a voice for young, Black males.
Tupac Speech about Thug Life
With all of the information that we at AllHipHop.com have uncovered as pieces of the Biggie and Tupac murders come to the surface, it’s important to remember that no matter how much we loved ‘Pac, and no matter how much we learn about his life post-humously, we still can’t bring him back to this life.  As the holograms proved earlier this year at Coachella, Tupac can never be duplicated, as close as some may come to recreating his persona. Perhaps ‘Pac and Biggie were Hip-Hop’s lesson to be better to the ones that are here to entertain us as musicians. Today, remember ‘Pac, but also remember Biggie, remember Whitney, remember Michael Jackson, remember Dilla, remember MCA, and all of the artists that gave their lives to this artform we call music.
And, as we remember Tupac Shakur on September 13, 16 years after he was gunned down, assassinated in the streets of Vegas, let’s stop and think about how ‘Pac would have wanted us to live our lives, and in turn, he will live through our actions forever. Tupac’s spirit will never die, no matter how many times he was shot in his final moments here on earth, because the legacy of his iconic aura lives on through generations of fans impacted by his songs. Icons don’t die, they live on even beyond their time on earth, and if that is true, we can safely say…
…heaven does have a ghetto.
“I Wonder if Heaven Got a Ghetto”
With that, we leave you will a few quotes from the seventh and final member of Tupac’s protege group the Outlawz, Young Noble. Being as close as he was to Tupac himself, let his words bring you a little closer to the man that taught us that “roses grow from concrete.”
What are your thoughts on the government’s role in ‘Pac’s murder?
Young Noble: “You gotta think, you know even prior to that [media scrutiny/harassment], with his family history, his mother being a Black Panther, and his uncle was Geronimo Pratt, Mutulu Shakur who really shook the country, like they are in the history books for this sh*t, people who you can Google and see what they were about back in the Panther day. The government knew that, and thought that he was a threat, he was awakening the people that they didn’t want awoke, and he was awakening the conscious mind.
“To be honest, it’s a lot of stuff that the world doesn’t know that’s not meant to be talked about in interviews, but at the end of the day, as far as the government finding out who killed ‘Pac, I never expected that. He threw up the middle finger at every chance that he had to at the establishment, but Tupac didn’t have a chance to have no peace in his life.”
In your eyes, what is the legacy of Tupac, not only on the West Coast, but in Hip-Hop?
Young Noble: “‘Pac belongs to the world; he was bigger than the Outlawz, his family, and the music. ‘Pac belongs to the world. We have to sit back and really embrace that. There’s so much about ‘Pac out there, that if you look at everything that’s out there as far as evidence, it will drive you crazy, and none of that is going to bring ‘Pac back. So we just have to live our lives how ‘Pac would want us to live and make him proud. He would want us to raise our kids, stay out of jail, and stay alive by any means necessary. Raise our kids right, and do what we gotta do.” Source allhiphop.com.

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LAFANA DODOMA


Msanii anayetamba katika miondoko ya R&B hapa bongo, Ben Paul akiwarusha wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika jana usiku kwenye uwanja wa Jamhuri.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah kutoka THT akitumbuiza jukwaani wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini Dodoma.

Anaitwa Recho kwa jina la kisanii kutoka nyumba ya vipati THT,akiimba jukwaani kwa madaha kabisa.

Msanii Rich Mavoko akiwapagawisha mashabiki wakati wa tamasha hilo


Msanii wa bongofleva aitwaye Shetta akiwaimbisha washabiki wake.Inatoka kwa mdau.

ZANTEL YAINGIA MKATABA NA AFRICAN LYON


Ofisa Mkuu wa Biashara wa Zantel, Sajid Khan akimkabidhi jezi, Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo kwa niaba ya klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam, katika hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro), Dar es Salaam wakati wa kutangaza kuingia mkataba wa kudhamini klabu hiyo kwa miaka mitatu. Wanaomfuatia Thadeo ni Meneja Mkuu wa African Lyon, Rahim Kangezi ‘Zamunda’ na Charles Otieno, Mkurugenzi wa Ufundi wa African Lyon. Kulia kabisa ni mchezaji chipukizi wa Lyon, Jarufu Magesa, ambaye anapelekwa na klabu Marekani kusoma. Lyon itashuka dimbani jioni hii kumenyana na Simba SC katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
CHANZO CHA HABARI: BIN ZUBEIRY

Simba Jana ili weza kugalagaza Vibaya African Lyon mabao 3-0


MABAO yaloyofungwa na Emmanuel Okwi, Daniel Akuffour na nassoro Cholo jana yaliwawezesha mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Simba kuanza vyema kutetea taji lao baada ya kuibamiza African Lyon mabao 3-0 katika moja ya mechi za ufunguzi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati Simba iliibuka na ushindi huo mnono wa mabao, watani wao wa jadi Yanga walishindwa kufurukuta mbele ya Prisons baada ya kulazimishwa kutoka nayo suluhu katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Okwi alikuwa wa kwanza kuitungua Lyon baada ya kuingia na mpira ndani ya eneo la hatari la Lyon, akawatoka mabeki wawili na kupiga shuti la mguu wa kushoto lililotinga wavuni. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Akuffour aliiongezea Simba bao la pili baada ya Okwi kuangushwa ndani ya eneo la hatari wakati alipokuwa akienda kusalimiana na kipa Abdul Seif wa Lyon.

Bao la tatu lilifungwa na beki Cholo, kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Mrisho Ngasa, ambaye alikuwa nyota ya mchezo kwa Simba.
Lyon ilipata nafasi nzuri ya kufunga bao wakati ilipozawadiwa penalti kipindi cha kwanza, baada ya Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, lakini shuti la Sunday Bakari liligonga mwamba wa pembeni wa goli.

MATOKEO MECHI ZOTE LIGI KUU LEO
Simba 3-0 African Lyon
Kagera Sugar 0-1 Azam FC
Prisons 0-0 Yanga
Coastal Union 1-0 Mgambo JKT
Toto African 1-1 JKT Oljoro
Polisi Moro 0-0 Mtibwa Sugar

JKT Ruvu 2-1 Ruvu Shooting.Inatoka kwa mdau.

Friday, September 14, 2012

WANAFUNZI 23 WA SHULE YA MSINGI KAPUNGA WANUSURIKA KIFO BAADA YA KUOKOTA MIKATE INAYOSADIKIWA KUWA NA SUMU.



The President extends his warmest wishes to all those celebrating the Jewish HIgh Holidays.


Ni katika shamba la Kapunga Rice Project.

Wazazi wacharuka na kuanza kujenga shule mpya mahali alipobomoa mwekezaji.
Zaidi ya shilingi milioni 2.5 zachangwa papo hapo.

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.

Wanafunzi 23 wa Shule ya Msingi Kapunga,Kijiji cha Mapogolo,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya kula mikate inayosadikiwa kuwa na sumu mnamo mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Ramadhani Nyoni na mzazi mmoja wapo wa watoto waliokumbwa na janga hilo la kusikitisha na kuhatarisha uhai.

Mzazi huyo ambaye hakupenda jina lake kutaja amesema yeye ilimlazimu kununua lita 20 za maziwa,kisha kuwanywesha watoto hao na kuokoa maisha yao ambapo hali zao zimetajwa kuendelea vema.

Wakazi wa kijiji hicho wakionekana kukerwa na kitendo hicho iliwalazimu kuitisha mkutano wa hadhara na kuazimia kujenga shule mpya ili kuwaondoa watoto katika shule iliyopo katika shamba la mwekezaji.

Mbali ya wananchi kukerwa na vitendo vya kikatili vya mwekezaji huyo,pia Walimu wamefurahia uamuzi wa wanakijiji kuamua kujenga shule mpya katika himaya ya kijiji ili kuondoa adha ya kutembea umbali wa kilometa 52 kwenda na kurudi kutoka Chimala,ambako ndipo walipopanga kutokana na uhaba wa nyumba kijijini hapo na zilizopo shambani kwa mwekezaji walimu hao hufukuzwa mara kwa mara.

ZIARA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA WILAYANI UKEREWE


Waziri Mkuu, Mizengo Pinnda na Mkewe Tunu (kushoto) wakivuka katika Pantoni ya MV Ujenzi kutoka Kisorya hadi Rugezi Ukerewe wakiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza Septemba 11, 2012. Aliyekaa kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina.

Wasanii wakitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Getreude Mongella mjini Nansio akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza, Septemba 11, 2012.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Viongozi wa Wilaya ya Ukerewe baada ya kuwasili Mjini Nansio kwa ziara ya kikazi Septemba 11, 2012. Kushoto ni Mkuu wa WIlaya hiyo, Mary Tesha.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WATANZANIA BARA KUPEWA VITAMBULISHO VYA WAGENI KISIWANI ZANZIBAR


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame MwadiniWatanzania bara wanaoishi Zanzibar wataanza kusajiliwa na kupewa vitambulisho maalum sawa na raia wa nje ya Tanzania wanaoishi Zanzibar.

Kwa Mujibu wa muswada wa marekebisho ya sheria ya Usajili ya Mzanzibari mkaazi namba 7 ya mwaka 2005 kazi ya kuwasajili itaanza kufanyika miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.

Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, Oktoba 10 mwaka huu.

Kifungu cha 6A (1) cha muswada kimeleza kwamba kila mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kujisajili katika Ofisi ya usajili wa vitambilisho vya Mzanzibari mkazi.

Muswada huo umeleza kwamba zoezi hilo pia litawagusa raia wa kigeni ambao wanaishi Zanzibar na kufanya kazi au biashara.

Kifungu cha 6A (3) kimeleza aina ya wageni wanaotakiwa kusajili kwa mujibu wa sheria hiyo wanaofanyakzi Zanzibar ama kwenye taasisi ya umma au binafsi pamoja na wanaofanyabiashara visiwani humo.

“Muajiri wa mkazi asiyekuwa Mzanzibari atatakiwa kutoa taarifa za mtu huyo kwa mkurugenzi au afisa msajili ndani ya siku 60 kuanzia ajira yake au ikiwa ameajiriwa kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii,” umesisitiza muswada huo.

Aidha, muswada huo umefuta kifungu cha 7 na watu wote watakaosajiliwa watatakiwa kuchukuliwa alama za vidole badala ya kidole gumba kimoja kwa mujibu wa sheria hiyo.

Akizungumza na NIPASHE Mkurugenzi wa usajili wa Vitambulisho vya Uzanzibari mkazi Mohamed Juma Ame, alisema serikali imeamua kuwasajili watu hao baada ya kubainika kuwepo watu wanaopewa vitambulisho hivyo kinyemela.

Alisema kwamba hali hiyo imekuwa ikifanyika baada ya vitambulisho hivyo kuonekana kuwa ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku hasa katika upatikanaji wa huduma za jamii.

Mohamed alisema sheria hiyo pia itasadia kuwatambua watu wanaoingia na kutoka Zanzibar maeneo wanayoushi na kazi wanazofanya Zanzibar.

Hivi karibuni Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi Zanzibar wameshindwa kunufaika na ajira katika sekta ya Utalii kutokana na kazi hizo kuvamiwa na wageni kutoka nje ya Zanzibar ikiwemo Tanzania bara.

SOURCE:IPPMEDIA

Kero na ghadhabu juu ya filamu katika nchi za Kiarabu





Maandamano nje ya Ubalozi wa Marekani nchini Misri
 
Kumezuka ghasia zaidi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kati ya polisi na waandamanaji wanaokashifu filamu ambayo wanasema kuwa inakejeli imani ya Kiislamu.
Runinga ya Misri ilionyesha gari likiteketezwa moto na watu wengine wakikimbia vitoza machozi.
Waandamanaji walitaka kufukuzwa kwa balozi wa Marekani nchini humo huku polisi wakiwafyatulia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.

Nchini Yemen waandamanaji wamevamia ubalozi wa Marekani wakichoma moto magari kabla ya vikosi vya ulinzi kuwadhibiti kwa kuwafukuza kutoka eneo hilo.

Maandamano zaidi pia yamefanyika katika nchi za Tunisia, Morocco, Sudan, Mauritania na Iran.

Wakati huohuo maafisa wa Marekani wanasema serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne kwenye ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni ya kupangwa au la .

Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa .

Maafisa wa Marekani wameelezea mashambulio hayo kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba makundi ya jihad huenda yalihusika .

Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa na uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed.

Takriban waandamanaji mia mbili wamekusanyika karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kwa usiku wa pili kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .
Awali waandamanaji walirusha mawe kwenye ubalozi huo na vikosi vya usalama vikafyatua mabomu ya kutoa machozi kuwa tawanya.

Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti walichomo moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao walizingira eneo hilo.

Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika

Exclusive: Brandy Champions Frank Ocean, Calls Dawn Richard the ‘Future’




The countdown is on to Brandy’s sixth album Two Eleven. After dropping two singles and releasing the tracklisting, the R&B diva is ready to make her much-anticipated return on October 16.
In Part 2 of our exclusive interview, Brandy opens up about working with Frank Ocean before he was a superstar. “I could see it then,” recalls the 33-year-old, who collaborated with the acclaimed singer-songwriter on “Scared of Beautiful.” “I’m just really proud that we are blessed by his talent.”
Another singer who’s earned her respect is Dawn Richard. “Dawn’s the future,” says Brandy, who has already spoken with the former Dirty Money member about a duet. “I just want her to get the credit that she deserves.”
While her joint tour with Monica never materialized, she is looking forward to launching her own tour in the near future. Plus, find out happened to her collaboration with Drake and which song she wants as her next single.

Wednesday, September 12, 2012

WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI NA BARABARA YA KILWA, ASEMA WATAKAOSABABISHA UJENZI CHINI YA KIWANGO KUFUKUZWA KAZI


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akijiridhisha kwa kupima kiwango cha lami inayowekwa upya katika barabara ya Kilwa na Kampuni ya Kajima ya Japan leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki, Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaki Okada na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Kajima.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (mbele) akiwa amefuatana na balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na viongozi wengine wa wizara akikagua moja ya sehemu ya barabara ya Kilwa inayojengwa upya na kampuni ya KAJIMA ya Japan kutokana na barabara hiyo iliyokamilika hapo awali kuwa chini ya kiwango na serikali ya Tanzania kuikataa na kuiagiza kampuni hiyo iijenge upya kwa gharama zake.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (katikati)akimweleza jambo balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada (kushoto) wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kilwa inayojengwa upya na kampuni ya KAJIMA ya Japan leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu waziri wa Ujenzi wa Ujenzi Gerson Lwenge.

Mhandisi mkazi wa Kampuni ya Kajima ya Japan inayojenga upya barabara ya Kilwa Hisashi Muto(kushoto) akitoa maelezo ya awali ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa pili kutoka kulia) Mbunge wa Kigamboni Dkt.Faustine Ndugalile (wa tatu kutoka kulia) leo jijini Dar es salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na kampuni ya China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni 214 na linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015.

Daraja la Kigamboni likiendelea kujengwa katika bahari ya Hindi eneo la Kurasini. Daraja hilo litakapokamilika litakua na njia 6 pamoja na barabara za juu na kuwa moja ya Daraja kubwa na la kipekee Afrika mashariki na kati.

Mmoja wa wafanyakazi wa daraja hilo ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiendelea na zoezi la kupiga picha huku akiwa amesimama kwenye mtando unaopitisha umeme mwingi bila kuchukua tahadhali wakati waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo leo.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, (CPA Africa Region) wamekutana kujadili mipango mbalimbali ya umoja wao, Mjini Colombo Sri Lanka


Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa CPA Africa akitambulisha ujumbe wa Tanzania (hawapo pichani) na baadhi ya Maafisa waliohuduria mkutano huo mjini Colombo Sri Lanka. Ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Mhe. Anne Makinda, Spika wa Bunge, Mhe. Zitto Kabwe, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Hamad Rashid Mohamed, na Mhe. Muhonga said Ruhwanya. Waliosima wa Kwanza kulia ni Ndg. Said Yakubu, Afisa Dawati wa CPA Tawi la Tanzania na Kaimu Katibu wa CPA kanda ya Afrika Ndg. Demitrius Mgalami.

Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, (CPA Africa Region) wamekutana kujadili mipango mbalimbali ya umoja wao katika Mkutano wa 58 wa CPA Dunia unaoendelea Mjini Colombo Sri Lanka. Pamoja na Mambo mengine, Kanda hiyo ya Afrika imejadili namna ya kuimarisha chama hicho, pamoja na maswala mbalimbali ya kiutendaji ndani ya Chama hicho ikiwa ni pamoja na msimamo wa Afrika katika maswala kadhaa ndani ya chama hicho duniani.

AMSHA AMSHA YA TWANGA PEPETA NDANI YA IRINGA NA MBEYA


Baadhi wa wanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta.

Bendi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta itakuwa na ziara ya maonyesho ya siku tatu katika mikoa ya Iringa na Mbeya.
Siku ya kwanza Twanga Pepeta inataraji kufanya onyesho mkoani Iringa tarehe 14-09-2012 siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Highland.
Kesho yake siku ya Jumamosi tarehe 15-09-2012 watakuwa Jijini Mbeya ndani ya City Pub na siku ya Jumapili tarehe 16-09-2012 watamalizia kufanya ziara ya maonyesho katika ukumbi huo huo wa City Pub kwa kufanya Bonanza maalum kwa ajili ya wakazi wa Jiji la Mbeya na maeneo ya jirani.
Matayarisho yote muhimu ya ziara hii ya maonyesho yamekamilika na Bendi inataraji kuondoka mara baada ya kumalizika kwa onyesho la kila siku ya Alhamisi tarehe 13-09-2012 linalofanyika Club Maisha Oysterbay.
Bendi inataraji kurudi mara tu baada ya onyesho la mwisho litakalofanyika siku Jumapili tarehe 16-09-2012 Jijini Mbeya.
Twanga Pepeta itakapokuwa katika ziara, Itamtambulisha Mwimbaji wao mpya Kalala Jr aliyerejea hivi karibuni kutoka katika Bendi ya Mapacha Watatu.
Sambamba na utambulisho huo pia itatambulisha nyimbo zao mpya za “Ngumu Kumeza” ilyotungwa na Mirinda Nyeusi, “Nyumbani ni Nyumbani” iliyotungwa na Kalala Jr, “Walimwengu” iliyotungwa na Jumanne Said na ” Mapambano ya Kipato” iliyotungwa na Mwinjuma Muumini.
Mara baada ya kurejea Twanga Pepeta itaendelea kufanya maonyesho yake kama kawaida Jijini Dar es salaam katika kumbi za Club Billicanas siku ya Jumatano, New Club Maisha siku ya Alhamisi, Free Time Resort Ukonga Banana, Mango Garden siku ya jumamosi na Jumapili mchana Leaders Club na usiku Mzalendo Pub.
MUDDY K
EVENTS MANAGER
TWANGA PEPETA.

WEMA ALIZWA TENA


Musa Mateja, Dar es Salaam BEAUTIFUL Onyinye wa Bongo, Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alijikuta akipata wakati mgumu baada ya kukombwa vioo vya gari lake aina ya Toyota Mark X na vibaka wa Moshi, Kilimanjaro, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Chuo cha Ushirika ambapo staa huyo alikuwa amehudhuria uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Akiwa katika burudani hizo, Wema ambaye muda mwingi alionekana kuwa mtu mwenye furaha ghafla alibadilika na kuishiwa na furaha alipolikuta gari lake likiwa limekongolewa vioo vyote vya pembeni.


Gazeti hili lilizungumza na Wema kuhusu tukio hilo ambaye alionekana kushangazwa na tukio hilo na kusema kuwa hakutarajia kukutana nalo kwa kuwa alikuwa akiwaheshimu sana watu wa Moshi.
“Imeniuma sana baada ya kukuta gari langu limekongolewa, wameiba vioo na ukiangalia nipo ugenini, halafu magari ni mengi yaliyokuwa yamepaki uwanjani, kwa nini yasiibiwe hayo mengine wakaiba langu tu, dah! imenikera sana,” alisema Wema kwa uchungu.
Hilo ni tukio lingine la Wema kulizwa, alishawahi kuibiwa nyumbani Sinza jijini Dar baada ya wezi kuruka ukuta na kumkomba baadhi ya vitu vya thamani, pia alishawahi kuibiwa vitu vingine ndani ya gari Uwanja wa Taifa.Inatoka kwa mdau.

WAMBURA BADO AIPASUA KICHWA TFF


Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Septemba 10 mwaka huu) ili kupitia na kutoa uamuzi/ushauri kwa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa mbele yake.

Wajumbe sita kati ya saba waliopo walihudhuria kikao hicho chini ya Mwenyekiti Alex Mgongolwa. Wajumbe hao ni Hussein Mwamba, Imani Madega, Ismail Aden Rage, Llyod Nchunga na Omari Gumbo.

Suala la ugombea wa Michael Wambura katika FAMMichael Wambura aliomba uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) katika uchaguzi uliofanyika Novemba mwaka jana.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliondoa jina lake kwa kukosa sifa ya kugombea nafasi hiyo. Wambura hakuridhika na uamuzi huo akapeleka shauri lake Kamati ya Nidhamu ya TFF. Kamati hiyo katika uamuzi wake ilisema haina mamlaka ya kushughulikia shauri hilo. Baadaye Wambura alikata rufani katika Kamati ya Rufani ya TFF ambayo ilimpa haki ya kugombea.

Kutokana na mkanganyiko huo wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwa na uamuzi wa mwisho katika masuala ya uchaguzi ya wanachama wa TFF, na uamuzi wa Kamati ya Rufani kuhusu uchaguzi wa mwanachama wa TFF, Sekretarieti ya TFF iliomba mwongozo wa kisheria kwa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji.

Kwa vile Kamati hizo mbili (Uchaguzi na Rufani) haziko katika mtiririko wa moja kwa moja wa utoaji maamuzi, Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliishauri Sekretarieti ya TFF kuliandikia Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ili kupata muongozo juu ya suala hilo.

Katika muongozo wake, FIFA ilitoa maoni kuwa kwa mujibu wa Katiba ya TFF chombo cha mwisho cha rufani katika masuala ya uchaguzi kwa wanachama wa TFF ni Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Hata hivyo, FIFA ilishauri kuwa si vizuri chombo kimoja kikawa msimamizi wa uchaguzi, na chenyewe tena ndiyo kiwe cha mwisho katika uamuzi kwenye uchaguzi husika.

Hivyo, Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji imetoa mapendekezo mawili kwenda Kamati ya Utendaji kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ili kiwepo chombo kingine cha rufani pale mgombea anapopinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Mapendekezo hayo ni; Iundwe Kamati ambayo itakuwa inasikiliza rufani zote zinazotokana na uamuzi uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, hivyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF isiwe chombo cha mwisho cha uamuzi kwa rufani zinazotokana na uchaguzi wa wanachama wa TFF. AU. Rufani zote zinazotokana na uchaguzi wa wanachama wa TFF zisikilizwe na Kamati ya Rufani ya TFF. Kwa maana hiyo Kamati ya Rufani ya TFF ndiyo kiwe chombo cha mwisho kwa wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwasilisha malalamiko yao.Inatoka kwa mdau.

RECHO: MCHUMBA WANGU AMEYABADILI MAISHA YANGU




MWANADADA Rachel Haule ‘Recho’ amekiri kuwa, tangu alipoanza kuishi na mchumba wake, George Saguda, maisha yake yamebadilika.
Mchezaji filamu huyo machachari alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, maisha ya kuwa msela na kuishi na mwenza wako yana tofauti kubwa.

“Tangu nilipoanza kuishi na Saguda, nimeona mabadiliko makubwa kimaisha,”alisema msanii huyo mwenye umbo lililojaa vyema.

Saguda ni mmoja wa watayarishaji mahiri wa filamu nchini na alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Recho mapema mwaka huu.

“Nampenda sana Saguda kwa sababu kwa sasa yeye ni msaada kwangu kiushauri, kimawazo na kimaisha,” alisema Recho.

“Naweza kusema Saguda kanituliza kwani kwa sasa siwezi kufanya jambo lolote la kimaendeleo bila kushauriana na mwenzangu, tofauti na awali ambapo nilikuwa najiamulia kitu cha kufanya na hakuna wa kuniuliza,”aliongeza.

Kwa sasa, Recho na Saguda wapo katika mipango ya kufunga ndoa ili kuwa mume na mke.Recho ni mwenyeji wa mkoa wa Ruvuma na wakati alipojitosa kwenye fani hiyo, alikuwa akisakamwa na shutuma nyingi kuhusu aina ya mavazi aliyokuwa akivaa.

Mwanadada huyo mantashau alikiri kuwa, baada ya kuwepo kwenye gemu kwa muda mrefu, alijikuta akibadilika taratibu na hatimaye kuanza kuvaa mavazi ya staha.

“Unajua baada ya kufika mjini, nilitekwa na mji na nilikuja kucharuka zaidi baada ya kuanza kufahamiana na wasanii wa bongo movi, ambao mara zote walikuwa wakinishauri nivae nguo fupi ili kuleta mvuto zaidi,”alisema.

Recho alisema inawezekana kwa wakati huo alikuwa akijiona hana tatizo, lakini kutokana na tasnia ya bongo movi kukumbwa na matatizo mengi, naye alijikuta akiingizwa kwenye mkumbo.

“Sio kwamba nilitaka kuharibiwa, hapana, nilijikuta tu napenda kuvaa mavazi, ambayo rafiki zangu walikuwa wakiyavaa na kadri siku zilivyokuwa zinakwenda, nilizidi kuzoea,” alisema.

Mwanadada huyo alikiri kuwa, fani ya filamu imemwezesha kupata mafanikio makubwa kimaisha, ikiwa ni pamoja na kumtangaza na kumfanya ajulikane zaidi hapa nchini.Baadhi ya filamu alizoshiriki kuzicheza ni pamoja na Cindy, Life to Life, Loreen, Men’s Day Out na Unpredictable.

Amemtaja msanii Blandina Chagula ‘Johari’ kuwa ni miongoni mwa watu waliomfanya avutike kujitosa kwenye fani hiyo kutokana na kuvutiwa na uigizaji wake.

Recho alikanusha madai ya kuwepo kwa rushwa ya ngono kwenye tasnia ya filamu. Alisema inawezekana jambo hilo lipo, lakini tangu alipojitosa kwenye fani hiyo, hajawahi kukumbana na adha hiyo.

“Maprodyuza ambao nimefanya nao kazi, wanaangalia uwezo wangu na kunikubali,” alisema.

Recho amekiri kuwa, mara ya kwanza alipopewa nafasi ya kucheza filamu ya Mtoto wa geti kali, alipata wakati mgumu baada ya kutakiwa ampige busu mwigizaji mwenzake wa kiume na lionekane busu la kweli.

“Nilisumbuka mno. Ilikuwa changamoto kubwa na kusema kweli nilimsumbua sana muongozaji wa filamu hiyo,”alisema.

“Ikitokea kuna eneo ambalo natakiwa kumpa denda msanii mwenzangu kwa ajili ya kuonesha uhalisia, nitafanya hivyo kwa ajili ya sanaa lakini baada ya hapo hakuna kinachoweza kuendelea kwa sababu nina mtu wangu, tunapendana,” alisisitiza.

Recho alisema amekuwa akifanya mazoezi kila siku kwa lengo la kuutuza mwili wake. Alisema amekuwa akiamka saa 11:30 asubuhi na kila ifikapo saa 12:00, anakuwa mazoezini kwenye viwanja vya klabu ya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam.

Mwanadada huyo anapenda sana kula wali kwa maharage, muziki na kwenda kujirusha klabu. Ndoto zake kubwa ni kuwa mbunge ili aweze kuwatetea wanawake wenzake.

Con or Conspiracy: Are They Really Out to Get Us?



911
“Them Alphabet Boys got us under surveillance” – “Soul Survivor”, Young Jeezy
The National Council of Black Leaders recently held a public forum called “The Conspiracy to Destroy the ‘Hood. “ When the first speaker, Dr. Afrika Shabazz revealed tons of information exposing a genocidal plot against African Americans, the panelists just rolled their eyes and snickered in disbelief. However, when Leroy Johnson complained that somebody had sent his voter registration card to the wrong address, they became outraged and demanded an immediate federal investigation into voter suppression…
Although, most people won’t admit it, we all believe in conspiracies. This world is too jacked up to be an accident.
Americans have long grappled with alleged conspiracies, from who shot Abe Lincoln to whether or not Elvis Presley is still alive and working at the Wal-Mart in Memphis. The most interesting conspiracy theories, however, have centered around the ‘hood, whether it be a secret sterilization formula put in fried chicken, or clothing companies secretly owned by the KKK as Dr. Patricia A. Turner examined in her work, Heard It Through the Grapevine.
First, there’s the vote conspiracy.
A few years back activists sounded the alarm that the meter was about to run out on the African American right to vote unless somebody did something real quick. (I’m still not sure what that something was supposed to be?) This year, the panic term is “voter suppression,” as there is, supposedly, some master plan to stop Black people people from voting.
Newsflash! With our jacked up priorities, no secret plot is needed to keep folks from the polls. If Jay-Z decides to hold a free concert in Madison Square Garden on November 6, you can kiss 80,000 votes goodbye – automatically.
Then there’s the infamous “movie ticket conspiracy,” whereby movie producers warn Black folks to keep an eye on their ticket stubs so the box office rating points will go to Soul Plane Part 2 instead of the new Michael Moore documentary.
While these types of conspiracies are taken very seriously by some people, the more serious ones that deal with Black survival are written off as paranoid ramblings.
During the early ’90s, researchers such as Steve Cokley Zears Miles and Keidi Obi Awadu spent countless hours on Black college campuses and in bookstores sharing information on topics from “The New World Order “ to “Why AIDS is so prevalent in the Black community.”
Also, “The Conspiracy to Destroy Black Boys” was tackled by such master teachers as Dr. Jawanza Kunjufu and Dr. Asa Hilliard, who painstakingly tried to convince Black parents that the reason why Lil Tyrone couldn’t read wasn’t because he was dumb but because of a Western mis-educational system.
However, by the mid ’90s, the heyday of these lectures had passed, as African American-owned bookstores struggled to keep the lights on, and Black college kids had more important things on their minds, like who was gonna perform at the homecoming show.
However, interest picked back up after 9/11/01, courtesy of videos like Loose Change that questioned the government’s official report of the attack on the Twin Towers. Even rappers like Jadakiss begin to ask why.
More recently, there has been an interest in Hip-Hop conspiracies, whether it be the death of a famous rapper, government persecution, or a secret organization within Hip-Hop with a diabolical plan to brainwash the masses.
Although the murders of rappers Tupac Shakur and the Notorious B.I.G. happened over 15 years ago, Hip-Hop fans are still discussing conspiracy theories as though they happened yesterday. As Dead Prez once said on “Bigger Than Hip Hop”, “Who shot Biggie Smalls/ if we don’t get them/ then they’ll get us all.”
It is also strange how so many rappers, especially the ones who make politically conscious music like Nas and Lauryn Hill wind up owing Uncle Sam millions of dollars.
This mystery is not limited to Hip-Hop, as it has been alleged that the Feds have, historically, targeted Black entertainers.
James Brown wrote in his memoir, I Feel Good, “All of us who were Black and in the public eye were under intense surveillance, harassed by the IRS and subjected to all forms of underhanded activities.”
Although Redd Foxx was not known for overt political activism, according to Pat Thomas in his book, Listen Whitey, he funneled some of his “Sanford and Son” money to the Black Panther Party during the ’70s. Also, in his book, Black and Blue, Michael Seth Starr wrote that the comedian alleged that the IRS targeted him “because of his skin color.”
It has long been rumored that the Feds keep a close watch on Hip-Hop artists for criminal and/or political activities, but recently, it was revealed that they also keep an eye on the fans. According to recent news reports the white rap group, Insane Clown Posse, is threatening to sue the FBI for labeling their fans (The Juggalos) as a gang.
This is nothing new to the boyz in the ‘hood, as states such as North Carolina have a GangNet database where they keep information about children suspected of gang affiliation.
Perhaps the most popular Hip-Hop conspiracy now is the idea that there is a secret nefarious club in Hip-Hop in which admittance can only be gained through a secret initiation.
Whether this is true or not is debatable, but what is not debatable is that it seems that participating in the genocide of the Black community by either sellin’ crack or shootin’ somebody seems to be a prerequisite for getting a record deal.
Of all the Hip-Hop conspiracies, the least believable is the “somebody hacked my Twitter account” conspiracy that artists like Chief Keef (or their PR people) use when they get called out for tweetin’ somethin’ wreckless.
Maybe conspiracies are true. Maybe they ain’t.
However, the best way to counter any plots against us is to not focus on what “they” are doing to us but what “we” are doing to ourselves.
For instance, if there is a conspiracy to use 16-year-old rappers to promote Black-on-Black violence, the counterattack would be to use the anniversary of the death of Tupac Shakur (September 13) to demand an end to murder music.
Most importantly, conspiracies can only survive when the masses of the people are kept in a state of ignorance.
So the ultimate solution is what The Wu Tang Clan suggested on “C.R.E.A.M.”:
”…to teach the truth to the young Black youth.”
TRUTH Minista Paul Scott’s weekly column is This Ain’t Hip Hop, a column for intelligent Hip Hop headz. He can be reached at info@nowarningshotsfired.com, on his website NoWarningShotsFired.com, or on Twitter (@truthminista).Source allhiphop.com

‘STEVE R&B’ AREJEA BONGO BAADA YA KUWA ULAYA KWA MIEZI SITA AKIFANYA SHOW…!!


MSANII Steve R&B ambaye alitamba na ngoma kibao ikiwemo ‘One Love’, aliyomshirikisha Baby Boy, sasa amefunguka na kuzungumza na mtandao wa DarTalk, kuwa kitu kilichomfanya kuwa kimya ni kutokana na safari ndefu aliyokuwa nayo ya kimuziki nchi za Ulaya iliyodumu kwa takribani miezi sita.

Steve alisema kuwa katika safari hiyo alifanya show katika nchi nyingi kama Germany, Italy, Australia na Swaziland, ambako kote alifanya makamuzi ya hatari kwa ajili ya katangaza jina lake pamoja na taifa lake kwa ujumla.

Hata hivyo alisema kuwa anaamini mashabiki wake watakuwa wamemisi vitu vyake, na katika hilo anadai kuwa sasa amekuja na staili mpya ujio kwa ajili ya kuonesha kile alikifanya nje kwa miezi hiyo sita.

Aliongeza kuwa baada ya kurudi kuna ngoma ambayo ameshaifanya na inakaribia kwenda sokoni ambayo inakwenda kwa jina la ‘Radio’ ambayo ndani yake anapatikana Ommy Dimpoz.

“Mashabiki wangu wanaweza kusema nilikuwa kimya sana, kama unavyojua kila mtu anazungumza analojua, lakini ukweli ni kwamba nilikuwa kimya kwa sababu nilikuwa Ulaya ambapo nilienda kwa ajili ya show,” alisema.Inatoka kwa mdau.

‘BENJAMIN WA MAMBO JAMBO’ KUJA NA NGOMA MPYA ALIYOIPA JINA ‘SKENDO’…!!

MSANII anayepagawisha mashabiki wengi kutokana na sauti yake ‘Benjamini wa Mambo Jamo’, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Skendo’, ambayo itazungumzia namna watu wanavyitengenezea skendo kwa lengo la kujipatia umaarufu usiyo na maana.

Akizungumza na mwandishi wa DarTalk, alisema kuwa ngoma hiyo inakuja hivi soon na ipo katika mtiririko mzuri wa mashairi pamoja na ujumbe wake, kitu ambacho kinaashiria kuwa itafanya vizuri kwani kwa upande wake si msanii ambaye anatoa ngoma kila baada ya wiki mbili.

Msanii huyo aliwahi kutamba sana na ngoma ya yake ya ‘My Friend’, ambayo inazungumzia mambo mengi ya maisha na njisi ndugu yako anavyoweza kukumaliza kwa ajili ya pesa au kutaka kuwa juu ya yako.

“Mimi si msanii ambaye anatoa ngoma kila baada ya wiki kwani najua kusoma alama za nyakati hivyo napokuwa kimya huwa natafakari ni namna gani naweza kutoa kitu kizuri kwa ajili ya mashabiki wangu,” alisema.

Hata hivyo sasa msanii huyo ana kampuni yake ya kutengeneza video inayoitwa Promo Only ambapo pia matarajiao yake ni kuwa na kampuni kubwa zaidi ya atakayoipa jina la B.M.L, ambayo itahusika zaidi na video pamoja na audio.Inatoka kwa mdau.

‘DIAMOND PLATNUM’ ALIVYOPAGAWISHA MASHABIKI NCHINI KENYA…!!


)