skills za kitaa

Thursday, December 5, 2013

RAY: CHUCHU NDIYE MKE WANGU


 Stori: Brighton Masalu
SINEMA ya madai mazito dhidi ya mastaa wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’, Ruth Suka ‘Mainda’ na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtangazaji Frank Mtao kuchanganywa kimapenzi na Vincent Kigosi ‘Ray’ sasa inaendelea na mhusika mkuu Ray amefunguka na kueleza yake ya moyoni huku akisisitiza: “Chuchu ndiye mke wangu, tarajieni makubwa soon (hivi karibuni).”
Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, wikiendi iliyopita katika Viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na mechi kati ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Muvi, Ray aliwashangaa waandishi kwa kumshambulia kutoka kimapenzi na Chuchu.
Mwandishi wetu alianza kwa kumwuliza: “Ray magazeti yanaandika kuhusu wewe kutoka na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Mainda amezungumza mengi. Kukaa kwako kimya bila kufafanua chochote siyo kitu kizuri. Tafadhali, hebu zungumza japo kidogo kuhusu madai ya Mainda.”
RAY: Sikia nikuambie, huyo Mainda utoto unamsumbua. Haniumizi kichwa kabisa. Kuhusu Chuchu... si mmeshaandika? Endeleeni kuandika lakini soon mtashuhudia kitu kikubwa sana.

Chuchu Hans.
RISASI: Ni kitu gani hicho?
RAY: Niacheni na Chuchu wangu.... kifupi ndiye mke wangu na itawashangaza wengi. Halafu mimi nawashangaa sana. Yaani mimi kutoka na Chuchu mnakuzaaaa... mbona alivyokuwa na ma-boyfriend zake wengine hamkuandika? Kwa sababu ni Ray basi mkaona ni habari. Mimi ninavyojua Chuchu siyo mke wa mtu.

No comments: