Mshiriki wa Burundi, Hope Jumapili iliyopita aliibuka mshindi wa shindano la Tusker Project Fame msimu wa 6.
Hope aliwabwaga waimbaji wa Kenya, Amos na Josh waliokuwa kipenzi cha wengi na ambao waliaminika wangeweza kuwa washindi.
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shilingi milioni 5 za Kenya
(takriban shilingi milioni 100 za Tanzania) Hope hakuamini masikio yake
na alilala chini kwa furaha huku baadaye akionekana kutaka kuanguka kwa
butwaa kubwa aliyokuwa nayo na washiriki kumshikilia.
Mshindi huyo wa Tusker Project Fame 6 amejishindia pia mkataba wa
mwaka mmoja wa kurekodi chini ya record label ya Sony Music Africa.
Nafasi ya pili imekamatwa na Wakenya hao, Amos na Josh na kufuatiwa
na Daisy wa Uganda huku mwakilishi wa Tanzania, Hisia akikamata nafasi
ya nne.
Katika fainali hiyo, washiriki walioingia tano bora walitumbuiza
nyimbo zao wenyewe walizozirekodi na pia kuoneshwa video za nyimbo hizo.
No comments:
Post a Comment