Na Emmanuel Richard Makundi
Bunge nchini Uganda limepitisha muswada wa sheria tata kuhusu kupinga
vitendo vya ushoga nchini humo, sheria ambayo sasa itashuhudia mtu
atakayepatikana na hatia akitumikia kifungo cha maisha jela.
Waandamanaji mjini Kampala walipoandamana hivi karibuni kupinga vitendo vya ushoga nchini humo
Sheria hiyo imepitishwa na wabunge bila kupingwa kufuatia mjadala mrefu
uliokuwa bungeni kuhusu kupinga vitendo vya ushoga kufanyika kwenye
taifa hilo ikiwemo ndoa za watu wa jinsia moja.
wabunge wengi wameonesha kuunga mkono muswada huo huku wachache
wakipinga kwa kile walichodai ni kwenda kinyume na haki za binadamu
wakati huu ambapo dunia ni yautandawazi.
David Bahati ni mbunge nchini humo nayeye ndiye aliyewasilisha muswada
huo bungeni ili ujadiliwe akitaka kutungwa kwa sheria kali ambazo
zitazuia vitendo vya ushoga nchini Uganda.
Sheria hiyo imepitishwa wakati huu ambapo wanaharakati nchini Uganda
wamekuwa wakiwatetea watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga, ambapo
kupitishwa kwa sheria hii kunakuwa ni pigo kwenye harakati zao.
mbunge Bahati anasema hatimaye nchi ya Uganda imeweka historia kwa
kupiga marufuku vitendo vya ushoga ambavyo vimekatazwa na mila za
kiafrika pamoja na vitabu ya dini kwa hivyo kuidhinishwa kwa sheria hii
kutazuia mmomonyoko wa maadili nchini humo.
Kwa mujibu wa sheria hiyo sasa, mtu atakayepatikana na makosa ya
kujihusisha na vitendo vya ushoga atakabiliwa na kifungo cha maisha
gerezani.
sheria hiyo imepitishwa huku ikiwa imepita siku moja tu toka wabunge hao
wapitishe sheria ya kukataza wanawake kuvaa mavazi ambao yanakaribia
kuonesha maumbile yao ya siri.
Sourcer: kiswahili.rfi.fr
No comments:
Post a Comment