skills za kitaa

Thursday, December 5, 2013

BABY MADAHA APASUA JIPU: DIAMOND FUSKA!


Erick Evarist na Sifael Paul
ACHANA na mabifu yaliyotangulia, hili ni jipya kabisaa! Msanii wa sinema na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ameingia kwenye bifu zito na Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kudai staa huyo wa Wimbo wa Number One ni mzinzi ‘fuska’, Amani lina mkanda mzima. 
Bila kumung’unya maneno, mapema wiki hii, Baby Madaha alimvaa Diamond ambaye ni Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB) akimtuhumu kuwa na tabia za kifuska.
Baby Madaha alidai hata muziki anaoufanya Diamond kamwe hauwezi kulingana na mafanikio makubwa ya jina lake zaidi ya kubebwa na skendo tu.CHOKOCHOKO ZILIVYOANZA
Kupitia mitandao ya kijamii, ilivuja posti ambayo ilidaiwa kutoka kwa Baby Madaha ikimpaka Diamond kuwa siyo mwanamuziki kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye uwezo mkubwa, akitolea mfano Elias Barnaba wa THT.

No comments: