Ni baada ya kuifungia timu yake goli Sergio Aguero akishangilia
Sergio Aguero akishangilia
Walcott akishangilia goli lake dhidi ya man city
KLABU ya Manchester City imeonyesha ni
hatari kweli, baada ya jioni ya jana kuifumua Arsenal mabao 6-3 katika
mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika Uwanja wa Etihad.
Mabao ya City yamefungwa na Sergio
Aguero dakika ya 14, Alvaro Negredo dakika ya 39 Fernandinho mawili
dakika za 50 na 88 David Silva dakika ya 66 na Yaya Toure dakika ya 90.
Theo Walcott alirejea uwanjani kwa
mara ya kwanza leo tangu Septemba na akafunga mabao mawili ya Arsenal
dakika za 31 na 63, wakati lingine lilifungwa na beki Per Mertesacker
dakika ya 90
No comments:
Post a Comment