Inaonekana mambo yanazidi kurudi kwenye mstari kati ya
mastaa wawili Justin Bieber na Selena Gomez ambao kwa muda mrefu mapenzi
yao yamekuwa na drama ambazo zilionekana kuupasua moyo wa Selena Gomez,
na kutangaza mara kadhaa kuwekana kando.
Siku kadhaa baada ya kuzagaa ripoti kuwa mastaa hao wamerudiana,
wameonekana wakitoka pamoja na kwenda mapumzikoni Jumamosi, January 4.
Mfanyakazi wa SeasCape Beach Resort katika eneo la Santa Cruz,
aliiambia KSBW kuwa Bieber na Selena Gomez waliambatana na baba yake
Justin Bieber, Jeremy Jack na kwamba walilala katika eneo hilo na
kuondoka kesho yake asubuhi.
“We were so very excited. He came Saturday night and left Sunday
afternoon. He and his friend (were) riding his Segway through the
campground and toward Manresa (State) Beach. It was the best thing
ever.” Alisema mfanyakazi mmoja.
Hata hivyo, Bieber na Selena hawakutaka kufahamika kwa hiyo walivyaa
mavazi tofauti huku Selena akivaa wig kichwani ili iwe vigumu
kufahamika.Lakini mashuhuda waliiambia KSWB kuwa walipogundua kuwa watu wameanza kuwafahamu, walikimbia ili wakajifiche lakini wakiwa katika harakati za kukimbia wig la selena lilianguka na nywele zake ndefu nyeusi zilionekana.
No comments:
Post a Comment