skills za kitaa

Thursday, January 16, 2014

Msanii Maarufu Kenya akanusha taarifa zinazodai yeye ni mshauri wa Rais Kenyatta










Kufuatia ripoti zilizoenea hivi karibuni nchini Kenya zikidai kuwa ‘Kigeugeu hitmaker’ Jaguar ndiye mshauri wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwenye maswala ya yanayohusu vijana, mwimbaji huyo amekanusha taarifa hizo.
Jaguar ametweet akikanusha taarifa hizo na kudai kuwa safari zake kuitembelea Ikulu ya nchi hiyo huwa na lengo la kumtembelea rais Kenyatta kama rafiki yake.
Akiongea na mtandao wa Ghafla wa Kenya, Jaguar amesema kuwa wakati wowote ambapo Rais Kenyatta anapohitaji maoni yake kuhusu maswala yanayowahusu vijana nchini humo, huwa tayari kutoa maoni yake.
Mwimbaji huyo ambaye hivi sasa video ya wimbo wake Kioo imeshika vipindi vya burudani vya runinga Afrika Mashariki, amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia harakati za kuwainua vijana nchini Kenya.
 
.. Articles stating that I'm the President's youth advisor; My visits to state house are solely to see His Excellency as a personal friend.

No comments: