Ingawa Kanye West alisema mwaka jana mwishoni kuwa mwaka huu
2014 hatasema maneno mabaya kwa mtu yeyote, ameuanza kwa vitendo vibaya
baada ya kumporomoshea ngumi zaidi ya 30 kijana mdogo aliyemtukana mama
mtoto wake Kim Kardashian.
Shuhuda wa tukio hilo aliiambia TMZ kuwa kijana huyo aliyesemekana
kumtukana Kim Kardashian kwa maneno ya kibaguzi akimuita Kanye kuwa ni
n***er (a n***er lover) alijikuta akila kichapo kama anapigwa na
mwanamasumbwi baada ya kuketi kwenye kiti kwa dakika kadhaa huku
akidhani yameisha.
Shuhuda huyo amesimulia kuwa dakika chache baada ya kumrushia maneno
Kim Kardashian na kuelekea kwenye ofisi moja ambapo alikaa kwenye kiti,
Kim Kardashian na Kanye West waliingia kwenye ofisi hiyo huku Kanye West
akiwa amekasirika, na bila kusema chochote alianza kumpiga ngumi
akiulenga uso wake huku mrembo wake Kim Kardashian akishuhudia.
Imeelezwa kuwa kijana huyo alijitahidi kuuzuia uso wake kwa kuukinga
na mikono lakini hali ilikuwa tete kwa mvua za ngumi toka kwa Yeezy.
TMZ imeripoti kuwa mtu wa mapokezi alipiga kelele kwa nguvu akimtaka
Kanye amuache mtoto huyo ‘stop, stop’ lakini aliendelea. Wahudumu
wengine waliingilia kati na kumsukuma Kanye West ili asiendelee kumpiga
kijana huyo.
Baada ya tukio hilo Kanye West alitoka nje ya jengo hilo kivyake na
Kim Kardashian akaelekea kwenye ofisi nyingine kwa ajili ya kikao.
Kwa mujibu wa USA Today, Polisi wametoa tamko wakithibitisha kuwa
walipokea simu kuhusu tukio hilo na kwamba kijana huyo na watu wengine
walimtaja mtuhumiwa kwa jina la ‘Kanye West’, na kwamba maafisa wa
polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.
No comments:
Post a Comment