skills za kitaa

Tuesday, January 21, 2014

Msome hapa chini Alichokifanya Beyonce ikulu ya Marekani katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Michelle, Obama awafundisha wageni ku-dougie

Mama Blue Ivy, Beyonce Knowles alimuongezea sababu ya kutabasamu First Lady wa Marekani Michelle Obama kwa kupiga show nzuri ndani ya ikulu ya nchi hiyo katika sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa Jumamosi, January 18.
 Katika sherehe hiyo ambapo Michelle alikuwa anafikisha umri wa miaka 50, Beyonce alienda na mwanae Blue Ivy ambapo baada ya sherehe hizo alipost kwenye mtandao picha zinazomuonesha mwanae huyo akichezea vitu kadhaa ndani ya ikulu, na picha moja ilimuonesha akicheza na mbwa wa Obama, Sunny.
Wageni wengine waliohudhuria katika sherehe hiyo ni pamoja Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton, mwimbaji Mary J. Blige, John Legend, Paul MacCartney, Samuel L. Jackson, Stevie Wonder, Jennifer Hudson na wengine.
Inaripotiwa kuwa Barack Obama alitoa hotuba nzuri kwa ajili ya mkewe na kwamba kuna wakati alishuka kwenye dance floor na kujaribu kuwafundisha wageni jinsi ya ‘ku-dougie’.
Baada ya kupata live performance kutoka kwa wanamuziki walioalikwa, Dj Cassidy alichukua nafasi yake na kuchanganya nyimbo kwa ustadi kuwaburudisha wageni hao.

Chanzo: TimesFm Website: www.timesfm.co.tz

No comments: