Subira yavuta kheri na kheri imevutika nchini Uingereza.
Mkewe Prince William, Kate Middleton hatimaye kajifungua mwanawe wa
kwanza wa kiume ambaye pia atakuwa mtoto wao wa kwanza . Kate
alikimbizwa hospitali mjini London kwa gari akiwa ameambatana na
mumewe.(Photo dailymail.com)
Shangwe vifijo na hoi hoi zimetanda katika jiji la Uingereza na
vitongoji vyake baada ya mke wa mwana mfalme Kate kujifungua mtoto wa
kiume leo Jumatatu 22-07-2013 saa 10.24 jioni .Mtoto wa kifalme huyo
anaingia katika kizazi cha nne cha kifalme.
Kate, aliyejulikana awali kama Catherine Duchess wa Cambridge,
amejifungua mtoto huyo wa kiume katika hospitali ya St.Mary huko jijini
London. Mtoto huyo atakuwa wa tatu katika mstari wa kupata ufalme kutoka
kwa babu yake, mwana mfalme Charles, na Baba yake William.
“Mimi na mke wangu tunafuraha kubwa sana kwa ujio wa kuzaliwa mjukuu
wetu wa kwanza” alisema Charles kwenye tamko lilotolewa na msemaji wa
familia ya kifalme.
“ Maisha ya kuwa babu na bibi wa mjukuu ni ya kipekee sana katika maisha
ya mtu. Na leo nina furaha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza na
tunasubiria kwa hamu kubwa sana kumwona mtoto aliyezaliwa” Alisistiza
Charles kwenye tamko hilo.
Shangwe na hoi hoi zimesikika nje ya eneo la Lindo Wing ambapo ipo
hospitali ya St. Mary baada ya tamko hilo kutolewa. Watu wazidi
kumiminika kuelekea katika kasri ya kifalme kupate habari zaidi juu ya
ujio wa mtoto wa kiume aliyezaliwa.
CHANZO Sunday shomari na www.dailymail.com
No comments:
Post a Comment