Balozi mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na
Mexico Mhe. Liberata Mula mula akiwa na rais Barack Obama mara baada ya
kuwasilisha hati za utanmbulisho Siku ya Alhamis Julai 18, hapo White
house.
Mama Balozi Liberata Mula mula akipokelewa na mama Munanka baada ya
kukutana na rais Obama na kujitambulisha huko White house alhamisi .
Mchungaji Ferdinand Shideko wa Kanisa la The Way Of The Cross Gospel
Ministries Maryland nchini Marekani. akifungua kwa sala kwaajili ya
ufunguzi rasmi.
Balozi mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Nchi za Marekani na Mexico Liberata Mula mula akitoa shukurani za
dhati kwa mabalozi wenzake waliofika kumpongeza pamoja na Bw.EL na
waTanzania wote waliokuwapo kwa kuhudhuria hafla hiyo iliofanyika Siku
ya Alhamis Junali, 18 ndani ya ubalozi wa Tanzania Washington DC nchini
Marekani.
Alieleza pia kushangazwa kwake na mapokezi yasiyo na makuu yalio ya
kifamilia zaidi aliyopewa huko White house na Rais Barack Obama na
familia yake alipowasilisha hati zake za utambulisho siku ya alhamisi
Julai 18.
Mama Balozi Mula mula akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa bunge la Tanzania na mbunge wa Monduli Edward Lowassa.
Baadhi ya mabalozi wakipata picha ya pamoja na Mhe Balozi Mula mula, kwenye hafla hiyo iliofanyika Siku ya Alhamis Junali, 18 ndani ya ubalozi wa Tanzania Washington DC nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment