skills za kitaa

Tuesday, July 30, 2013

DJ Choka adai ngoma yake kubaniwa kwenye kituo kimoja cha Radio hapa TZ

DJ maarufu wa wasanii wa Bongoflava, DJ Choka amekasirishwa na kuamua kufunguka kupitia akaunti yake ya Twitter kuhusu kutopigwa kwa nyimbo zake (kumbuka anafanya muziki kama DJ Khaleed) kwenye moja ya Radio za hapa TZ.
Inavyoonekana DJ huyu ambaye anamsupport mwanadada Lady Jaydee amejikuta ameingia kwenye matatizo hayo baada ya kuwa upande huo wa #teamAnaconda. Kupitia akaunti hiyo DJ Choka aliandika:


Bado haijafahamika ni Radio gani na nani waliokataa kupiga nyimbo za DJ huyo kutokana na sababu walizozitoa, lakini unaweza ukajua tuu ni wale wale waligombana na Lady Jaydee.

Kwa sasa DJ Choka anatikisa na ngoma yake  Latino Nation  huku akiwa amewashirikisha wasanii wanaotoka label moja ya BHitz.

No comments: