Ingawa bado yako chini kulinganisha na nchi nyengine duniani, matumizi
ya intaneti nchini Somalia yanakuja juu kidogo kidogo huku kampuni
zikipigania wateja na raia zaidi wakiwa na fursa ya kutumia intaneti
katika nyumba zao na sehemu za biashara.
Vijana wa Kisomali wakitumia mtandao wa intaneti katika Mkahawa wa Amudi mjini Mogadishu. [Mahmoud Mohamed/Sabahi]
Idadi kubwa kampuni za simu nchini Somalia - kubwa zaidi zikiwemo Global
Internet, Golis Telecom, Telesom na Somtel - wanashindana kutoa huduma
za intaneti kwa wateja na mikahawa nchi nzima kupitia mitandao mbali
mbali ya minara, satalaiti, na mikonga ya mawasiliano.
"Mwaka wa 2000 watumiaji wa intaneti walikuwa chini ya asilimia 1 (ya
raia wote), lakini idadi imepanda juu kwa miaka ya hivi karibuni hadi
kufikia kiasi ya asilimia 2 katika mwaka wa 2011, kwa mujibu wa makisio
yasiyo rasmi," alisema Abdisalam Mohamed, mkurugenzi wa masoko wa Global
Internet, moja ya watoaji wakubwa wa huduma za intaneti katika eneo la
kati na kusini mwa Somalia.
Mohamed alisema kampuni mjini Mogadishu sasa zinatoa aina mbalimbali za
huduma za intaneti kwa watumiaji binafsi, kama vile DSL, huduma ya
intaneti isiyotumia waya na za satalaiti.
Licha ya upatikanaji wake, huduma za majumbani hazijawafikia Wasomali
wengi kutokana na ughali wake. "Gharama (za huduma) hizi ni kati ya dola
30 hadi dola 600 kwa mwezi, kulingana na kiwango cha huduma na kasi ya
kuunganishwa inayotumiwa na mtumiaji," alisema Mohamed.
No comments:
Post a Comment