WAKATI klabu za Yanga na African Lyon zikiendelea kusuguana namdhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kampuni ya simu ya mkononi yaVodacom, klabu za soka nchini zimeaswa kuanza kujitambua ili ziwezekunufaika kwa mambo mengi zaidi, badala ya kutumia muda mrefukulumbana kwa mambo madogo, akitolea mfano wa nembo ya Vodacom katikajezi za klabu.
Ushauri huo umetolewa na mfadhili wa zamani wa Simba, mfanyabiasharaAzim Dewji aliyesema kuwa, kama klabu za Tanzania
zingekuwazinajitambua, kamwe zisingepoteza muda kwa malumbano ya nembo, balimaslahi.
Akizungumza jana, alisema klabu kubwa kama Simba na Yanga, zinapaswakujenga hoja nzito kwa wadhamini, ili ziweze kunufaika zaidi kwa kuwazina thamani kubwa kutokana na ukongwe wake na utajiri wa wafuasi kotendani na nje ya Tanzania.
“Sawa wana haki, lakini klabu zetu ifike mahali zijitambue. Wavukehapo, mfano Simba na Yanga si zijenge hoja za kupata fedha zaidi kwawadhamini kwamba ili zivae jezi na nembo, zilipwe vizuri kulingana nahadhi halisi ya klabu hizi.
“Haiingii akilini kuona zimeshindwa kujenga ushawishi hata baada
yakuwekwa kundi moja na timu ambazo hazina wanachama wala ofisi, lakinikwa mujibu wa mkataba zote
zinalipwa sh milioni 7 kwa mwezi.
“Jamani, hivi Yanga yenye utitiri wa wanachama na wafuasi, utajiri
wamajengo mfano jingo lake lina thamani ya bilioni 2, inalipwaje sawa naAfrican Lyon ambayo haina wanachama wala ofisi?
“Si kama naidharau Lyon, la hasha, bali ndio uhalisia kwa sababu kamani kunufaika, Vodacom itanufaika zaidi kwa Yanga kutokana na wafuasiwake wengi kuliko Lyon, kwanini wasitumie mwanya huo kujenga hoja?”alihoji Dewji na kuongeza kuwa, hadhi ya klabu za Simba na Yanga angalau
kila moja iambulie sh milioni 250 kwa mwaka, na jezi za hadhiya juu kulingana na hadhi ya klabu
zenyewe.
Aidha, alisema udhamini mnono wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) niuthibitisho tosha kuwa thamani ya Simba na Yanga. TBL kupitia bia yaKilimanjaro, inazidhamini Simba na Yanga kila moja kwa wastani wa shbilioni 1.5 kwa mwaka, udhamini ukigusa mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi, mabasi, vifaa vya michezo, gharama za mikutano yakila mwaka na kadhalika.
“Una sasa, TBL si wadhamini wakuu wa soka ya nchi hii, lakini klabuhizi zinanufaika, kama ukweli ndio huo kwa nini wasimbane mdhamini waligi ili
wanufaike zaidi na badala yake wanabaki na malumbano ya nembopekee? Ni wakati wa klabu zetu kubadilika kwa sababu kote ulimwenguni,soka ni biashara kubwa mno,” alisema.
Kauli ya Dewji imekuja huku klabu za Yanga na Lyon zikiwa katikamgogoro juu ya kutovaa jezi zenye nembo ya Vodacom, Yanga ikisemahaiko
tayari kuvaa jezi zenye nembo nyekundu ya mdhamini huku Lyonikitaka iruhusiwe kuvaa jezi za mdhamini wake binafsi, kampuninyingine ya simu za mkononi ya Zantel.
Kutokana na mvutano huo, klabu hizo zimejiingiza katika hatari yakuadhibiwa, kwani Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetishia kuchukuahatua dhidi
ya klabu zinazokwenda kinyume na matakwa ya mkataba waudhamini wa Ligi Kuu ambao hata hivyo klabu zinalalamikia kuwa hauko wazi.Inatoka kwa mdau.
No comments:
Post a Comment