Emmanuel Shayo ambaye ni Mkurugenzi toka kampuni Maarufu ya Macmedia ya Jijini Dar es Salaam
amesema ameanza utaratibu wa kuchukua wasanii chipikizi kwenye muziki , filamu pamoja na urembo.
Ambapo hadi sasa tayari amepata wasanii ambao tayari wameingia studio kurekodi ngoma mpya zitakazoanza kusikika sikuza usoni , licha ya hao bado anakaribisha vipaji chipukizi na kutoa mkataba kati yake na vipaji hivyo.
Rosemary Silungwe ambaye ni mwanafunzi wa kidatocha sita Mbezi Beach High School ya Jijini
Dar es Salaam.
Silungweta yari ameonesha mafanikio ya mwanzo ambayo si haba kwa mwanzo wake wa kufikia majukwaa ya kimataifa.
Kwa sasa yeye ni miongoni mwa wenye vipaji vya urembo nchini heshima yake iliibuka baada ya
kushiriki kwenyetamasha lililoandaliwa na kipindi cha Flend of Flends kilipoandaa tamasha hilo Shuleni Mbezi Beach kinachorushwa hewani kupitia Luninga ya
East Africa Tv na sasa ataanza kufaidi kipaji chake hicho akiwa chiniya Macmedia Production.
No comments:
Post a Comment