skills za kitaa

Monday, October 8, 2012

DIAMOND APATA WASIMAMIZI WA KAZI ZAKE


MSANII nyota kwenye muziki wa Bongoflava  Diamond akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya I-View Studios, Raqey Mohammed baada ya kutia saini mkataba wa kusimamia kazi zake. Wengine pichani ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya, Mwanasheria wa I-View, Dr. Peter Aringo na
Mkurugenzi wa One Touch Solutions, Petter Mwendapole.

Nimekuwa nikipokea maoni mengi sana kutoka kwa watu mbali mbali,na moja ya jambo ambalo nilikuwa nikisistiziwa ni kuwa na Management yangu itakayokuwa ikiniongoza na kusimamia kazi zangu kwa ujumla. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu swala hilo limefikia tamati na sasa ni muda muafaka naiweka wazi Management yangu ni kampuni ya I-VIEW inayoongozwa na Raqey. Hao ndio watakuwa wakisimamia kazi zangu na kuniongoza nipite njia gani amabayo itakuwa ni salama zaidi. Ukweli ni kwamba hakuna binadamu anayeweza kufanya mambo yote ni lazima kuwe na watu wenye upeo mkubwa,watakaoweza kunisaidia baadhi ya mambo ili kuweza kufanya kazi zenye kiwango cha hali ya juu na niweze kuufikisha muziki wetu wa Bongo Flavour mbali. ( Ahsanteni sana,nawapenda sana mashabiki wangu)

No comments: