skills za kitaa

Tuesday, October 16, 2012

Mkoa wa Kaskazini Unguja watoa maoni yao Katiba mpya


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa mkutano ulioitishwa siku ya tarehe 13 Oktoba, 2012 na Tume hiyo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.

Wengine pichani (kutoka kulia) ni Wajumbe wa Tume hiyo, Joseph Butiku (kulia), Profesa Paramagamba Kabudi, Katibu wa Tume, Assaa Rashid na Naibu Katibu Casmir Kyuki
  
Wananchi wa Kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar wakifuatilia kwa makini mkutano ulioitishwa Siku ya  tarehe 13. Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo wenye malengo ya kukusanya maoni yao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba
Bw. Yusuph Juma (60) mkazi wa Kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa Siku ya tarehe 13. Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.
Bw. Said Haji Makame (21), mkazi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa tarehe 13. Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.
Bi. Tatu Maalim Mganga (65) mkazi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa tarehe 13 Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.
Habari na picha kwa hisani ya ZanziNews.Blog 

No comments: