Msanii wa hip hop Marekani 50 Cent amekuwa akiingia kwenye headlines
mbalimbali mara baada ya kutangaza kuwa amefilisika na safari hii
headlines zinazomhusu 50 Cent ni za yeye kutafuta mpangaji wa nyumba
yake iliyopo Connecticut Marekani.
Taarifa hizi zilianza kusambaa kwa fujo siku ya jumatano baada ya kukamilisha mkutano wake na Wanasheria.
Mwanasheria wa 50 Cent, Stephen Savva alisema japo hakuna mkataba wa upangishaji uliofikiwa kupangisha nyumba yake ya Farmington Mansion ambayo 50 aliinunua mwaka 2003
wamekuwa wakifanya mipango ya kupangisha nusu ya nyumba hio yenye
vyumba 21, majiko 9 na casino lakini mpaka sasa rapper huyo hajabahatika
kupata mpangaji.
Bado hatujasikia kiasi cha pesa ambacho msanii huyo atatoza kama kodi
ya nyumba, ila documents zilizowasilishwa Mahakamani zinasema kuwa 50
Cent amekuwa akilipa dola 72,000 (Tzs.Milioni 144) kwa mwezi tu kama
hela ya matunzo ya nyumba hiyo ambayo ni tofauti na kodi yake ya nyumba!
Duh! Unadhani hapa 50 Cent atapata mpangaji kweli kama matunzo yenyewe ndio hayo?
No comments:
Post a Comment