Ivory Coast iliishinda Ghana kwa mikwaju ya penati 9-8
Timu ya soka ya Ivory Coast imenyakuwa taji la Kombe la Afrika la
mwaka 2015 kwa kuitandika timu ya Ghana kwa mikwaju ya penati mjini
Bata, Equatorial Guinea.
Nahodha wa Ivory Coast akikabidhiwa kombe
Ivory Coast imeshinda kwa mikwaju 9 ya penati huku Ghana ikipata mikwaju 8.
Yaya Toure akishangilia baada ya kukabidhiwa taji lao
Boubacar Barry, 35, ndiye aliyeibuka kidedea kwa kufunga penati ya
mwisho baada ya mlinda mlango wa Ghana Razak Braimah kukosa penati.
Shangwe na vigeregere mjini Bata, Equatorial Guinea
Mlinda mlango mkongwe wa Ivory Coast Boubacar Barry ndiye nyota wa mchezo wa leo.
Mlinda mlango nambari mbili wa Ivory Coast ndiye aliyepia ushindi timu yake
Mwaka 1992, Ivory Coast waliifunga Ghana kwa mikwaju ya penati 11-10.
Ghana walipata penati 8 huku Ivory Coast wakishinda kwa penati 9
Mashindano hayo yalikuwa yanafanyika nchini Equatorial Guinea.
No comments:
Post a Comment