Kesho
Jumapili, Yanga itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kimondo FC ya Mbeya, timu
hiyo imepania kuonyesha soka safi kuthibitisha ubora mbele ya winga wao wa
zamani, Geoffrey Mwashiuya aliyejiunga na Wanajangwani.
Yanga inatarajiwa kuondoka jijini
Dar es Salaam, leo Jumamosi tayari kwa mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa
CCM Vwawa, Mbozi jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake kwa msimu ujao
wa Ligi Kuu Bara.
Mchezo huo ni sehemu ya makubaliano
ya kimkataba ya uhamisho wa Mwashiuya aliyejiunga Yanga na kugeuka lulu
kutokana na uwezo wake kuwavutia wengi.
Ofisa Habari wa Kimondo, Chriss
Kashililika amesema timu yao ina jeuri ya kuifunga Yanga kwa kuwa ina kikosi
imara kwani ina wachezaji wanaofanana kiuchezaji na Mwashiuya zaidi ya nane.
“Maandalizi ya mchezo yapo vizuri
kwa sababu timu ipo kambini, Yanga ni timu kubwa na tunaiheshimu lakini kwa
jinsi tulivyojipanga kwa mchezo huo uhakika na ushindi ni mkubwa.
“Kama Yanga walidhani wametukomoa
kwa Mwashiuya basi wanajidanganya, tuna kina Mwashiuya kama nane, kwa hiyo
pengo lake limezibika na tutafanya vizuri,” alijigamba Kashililika.
na Saleh Ally
na Saleh Ally
No comments:
Post a Comment