Nigeria imepigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya kandanda yanayoandaliwa na shirikisho la soka duniani FIFA.
Hatua hii imeafikiwa baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF afisini.
Marufuku hii inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini Nigeria inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa.
FIFA ilikuwa imeionya Nigeria kuwa ingeichukulia
hatua ifikiapo Jumanne kama Shirikisho la NFF halijarejeshewa madaraka
yao lakini Serikali ikapuuza makataa hayo.
Mwishoni mwa juma Serikali ya Nigeria ilikuwa
imemteua afisa mshikilizi kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi wa huru
na wa haki utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya michezo.
FIFA katika taarifa imeonya kuwa marufuku hiyo itaondolewa tu iwapo maafisa waliochaguliwa watarejeshwa mamlakani.
Marufuku hiyo itaathiri timu ya taifa ya Super
Eaglets ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 ambayo inapaswa
kushiriki mchuano wa kombe la dunia iwapo marufuku hiyo haitaondolewa
ifikapo juma lijalo.(Julai15)
Msemaji wa serikali hata hivyo alisema kuwa
hatua iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata kiongozi wa
shirikisho la soka la Nigeria Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde
baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil.
Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri
hakuwa anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo duni
huko Brazil.
Wajumbe wa NFF waliafiki kauli ya mahakama ya
kumn'goa mwenyekiti huo madarakani lakini lakini kwa sasa erikali ya
Nigeria inasubiri mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma ithibati ya
mkutano maalum uliofanyika na wajumbe wa shirikisho la soka la NFF .
Mabingwa hao wa Afrika walishindwa katika mkondo wa pili wa kombe la dunia na Ufaransa .
Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa timu hiyo kufuzu kwa mkondo wa pili baada ya kufuzu mwaka wa 1994 na 1998.
No comments:
Post a Comment