Waliokuwa
wamiliki wa Beats Eletronics Dr. Dre na mfanya biashara mwenzake Jimmy
Iovine wamefungua kesi ya madai dhidi ya mitandao na makampuni ya China
yaliyouza bidha feki kwa kutumia jina la bidha ya Beats Eletronics ya
Beats By Dre. Dr Dre akishirikiana na Apple wametoa taarifa kuwa mpaka
sasa bidha hizo feki zimetengeneza kiasi cha dola za Marekani bilioni
135.
Dr. Dre ambaye ameuza haki za bidha ya Beats headphones kwa Apple
anafanya bidii zote kuzuia bidha feki za China kuharibu bidha zake za
Beats By Dre. Tmz imeripoti kuwa kesi ya Dr Dre kwa mtandao huo ambao
haujatajwa ni kuzuia na kudai fidia walizo ingiza kupitia kuuza bidha
zenye logo ya Beats By Dre ambazo hazina kiwango cha bidha halisi na
hivyo kupotosha wateja na kuharibu jina la bidha yake.
Dr Dre akishinda kesi hii ya madai basi fidia atakayolipwa itamfanya awe billionaire.
No comments:
Post a Comment