Neymar amesafirishwa kwa helikopta kupelekwa Sao Paulo kuanza mapumziko
NYOTA wa Brazil, Neymar anaamini timu yake itashinda Kombe la Dunia bila ya kuwa na yeye.
Mchezaji huyo wa Barcelona aliaga mashineano hayo juzi usiku baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Colombia, Juan Zuniga.
Mchezaji huyo wa Barcelona aliaga mashineano hayo juzi usiku baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Colombia, Juan Zuniga.
Mchezaji
huyo ameelezea maumivu yake baada ya pigo hilo linalomuondoa Kombe la
Dunia mapema akiiacha timu yake imetinga Nusu Fainali na zaidi
amewatakia heri wachezaji wenzake wabakize kombe hilo nyumbani.
Neymar
amesafirishwa kwa helikopta baada ya tiba ya awali na kupelekwa Sao
Paulo kuanza mapumziko. Tayari FIFA imesema inalifanyia uchunguzi tukio
hilo kabla ya kumchukulia hatua Zuniga.
Neymar akipewa pole na Rais wa Shirikisho la Soka Brazil, Jose Maria Marin.
No comments:
Post a Comment