Muigizaji
wa filamu,Wastara Juma amewapa watu simamzi zito mtandaoni, baada ya
leo kuandika maneno mazito ya uchungu akisema matatizo ya dunia
yamemzidia na kubandika picha akiwa analia. Na hivyo kupelekea mashabiki
wengi kumpa pole na kumtia moyo kuwa yote yana mwisho wake na Mungu
ndio mpagaji wa yote.
"Hapa
duniani kila mtu ana shida na matatizo lakini kwangu mimi yamezidi daaah
eeeh Mungu nibadilishe basi hiyo nafasi ya mteso uliyoniweka muweke
mwingine nami unipe furaha nicheke kama wengine maishani mwangu niache
kulia eeeh Mungu baba jamani mimii mimiii aah".-Wastara aliandika baada
ya kuweka picha hiyo hapo juu.
Hakuweka wazi nini hasa kimempata,lakini picha hii inaonekana imetoka kwenye moja ya kipande cha filamu.
Chanzo:http://www.bongomovies.com/
No comments:
Post a Comment