Msanii wa bongo Fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee amefunguka na kuweka wazi kuwa katika maisha yake ya kawaida, maisha ya sanaa na maisha ya utafutaji amekuwa akikutana na changamoto mbalimbali.
Changamoto hizo wakati mwingine hupelekea watu kugombana au
kutofautiana kutokana na mtazamo au matatizo mbalimbali na amedai wazi
kuwa katika watu wote ambao aligombana nao na yeye kugundua ndiye
alikuwa chanzo cha ugomvi huo wote alishawaomba msamaha na wanaendelea
na maisha ya kila siku.
Lady Jaydee alisema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Instragram
wakati akijibu maswali 10 yaliyotokana na maswali kibao kutoka kwa
mashabiki wake.
“Nitapatana na mtu atakae kubali kuwa alikosa, kama naamini yeye ndio
alinikosea itabidi aniombe msamaha. Kama mimi ndio nilikosa nitaomba
pia msamaha Otherwise hakuna miujiza Siwezi kumuomba mtu msamaha endapo
naamini kabisa sijakosa .
Niliowahi kuwakosea nilishawaomba msamaha wooote.Hakuna binadamu asiye kosea ila siwezi ku surrender kiuongo au kwa uoga wa maisha.
Naamini hata nikiuza nyanya bado wapo watu wanaohitaji nyanya, na watanunua.”

Baadhi ya mashabiki waliuliza kwanini Lady Jaydee hana ushirikiano na
wasanii wenzake wa kike katika muziki na yeye aliweka wazi kuwa amekuwa
akishirikiana nao sana tu mpaka kufikia hatua wengine kuwatungia wimbo,
Jide anadai kuwa mara nyingi ili msanii aweze kutoka au kufanya vizuri
lazima kazi zake zipate promo ya kutosha katika vituo mbalimbali vya
Radio lakini bahati mbaya yeye sio mwenye hizo Radio.
“Nimewahi kufanya na wasanii mbalimbali wa kike ila sijui kwanini hamjaziskia.
1. Mwasiti amewahi kunishirikiisha
2. Nimewahi kumuandikia na kushiriki kuimba kwenye wimbo wa movements za Albino na Keysha
3. Nimewahi kumwandikia na kushiriki kuimba na Nakaaya Sumari
4. Nimewahi kumwandikia wimbo Patricia Hillary
5. Nimewahi kumshirikisha RAY C kwenye wimbo wangu toka Album ya Machozi unaitwa, Nimekubali na wapo wasichana mbali mbali waliopita Machozi Band na kujifunza kuimba leo mnawafahamu, Kumbukeni tu kuwa kutoka kwa mtu itategemea na nyimbo zake kuwa promoted redioni na mimi sio mwenye hizo redio .
Msaada pekee ni kushiriki kila ntakapotakiwa kufanya hivyo”

Lady Jaydee kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Forever ambao
amemshirikisha mdogo wake anaefahamika kama Dabo na pia mwanadada huyo
amepanga kufunguka mengine mengi katika kipindi chake kinacho ruka
eatv.tv
No comments:
Post a Comment