Familia ya Mbasha inaendelea kutengeteza vichwa vya habari, baaada ya
mchungaji maarufu nchini Gwajima kukanusha kuwa si baba wa mtoto wa
Flora Mbasha, mume wa muimbaji huyo wa injili Emmanuel naye ameibuka na
kudai kuwa hatambui chochote kuhusu kuzaliwa kwa mtoto huyo.
Mbasha ambaye pia ni muimbaji wa muziki huo wa injili amesema
anachojua ana mtoto mmoja wa kike anaeitwa Lizy mwenye umri wa miaka
kumi na hizo taarifa za Flora kajifungua anazisikia kwa watu wengine.
“Nina mtoto mmoja, nina mtoto mmoja anaitwa Lizy ana umri wa kama
miaka 10 hivi! Wewe ndo unanieleza mimi kama amejifungua, kama
amejifungua, ni jambo jema na la kumshukuru Mungu,” alieleza Emmanuel
Mbasha
Mbasha alikiambia kipindi cha SunRice Times Fc.
No comments:
Post a Comment