MSANII wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari hivi karibuni
alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa kuzindua albam mpya iendayo kwa
jina la Blessing yenye nyimbo kumi na mbili (12).
Albam hiyo ambayo ni albam yake ya pili ilizinduliwa jijini Arusha na
kuhudhuriwa na mashabiki wa muziki wake kutoka mikoa ya Arusha, Manyara
na Kilimanjaro.
Huku
akiungwa mkono na wasanii wenzake kutoka hapa hapa nchini na nje ya
nchi.
Uzinduzi huo ulipambwa na burudani kabambe kutoka kwa Hisia, G Nako,
Jambo squad wote kutoka Arusha, Naaziz kutoka Kenya, na Nakaaya mwenyewe
yote hiyo nikumpasapoti msanii mwanzao.
Akizungumza kwa furaha mwanadada Nakaaya Sumari alisema kuwa
anawashukuru sana wote waliokuja kumuunga mkono katika uzinduzi wake.
“Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kunipa sapoti ya nguvu kwani wa
lijitokeza kwa wingi, nimefurahi sana kwani huu ni mwanzo mzuri,”
alisema Nakaaya.
“Albam
hii imebebwa na wimbo wa Blessing ambao ni maalum kwa mwanangu kipenzi
kwani yeye ni Baraka kwangu hata napokua mbali naye bado nakua na
matumaini na faraja,” Nakaaya aliongeza kwa msisitizo.
Albam ya Blessing ipo sokoni sasa na inanyimbo nzuri za kuelimisha,
kuburudisha na kuliwaza kama vile Utu uzima dawa, Temana na watu,
Blessing, Beautiful, I am an African, Sister sister, Ngufurie, na
Mwanamke shujaa, kubwa ni kumpa sapoti kwa kununua albam hii.
No comments:
Post a Comment