Mafuriko kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
Mabadiliko ya
tabia nchi duniani huenda yakaleta madhara makubwa zaidi na ambayo
hayawezi kurekebishika, ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya. Wanasayansi na maafisa wanaokutana nchiniJapan wamesema ripoti hiyo imefanya uchunguzi wa kina kwa sasa kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi duniani.
Wajumbe
wa jopo la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya hali ya hewa, wamesema
ripoti hiyo inatoa ushahidi wa kutosha wa kiwango cha madhara hayo.
Mifumo asilia kwa sasa haufanyi kazi sawasawa, lakini ongezeko la madhara kwa binadamu ndilo jambolinalohofiwa zaidi.
Afya zetu,
makaazi, chakula na usalama vyote viko katika hatari kutokana na
kuongezeka kwa viwango vya joto, ripoti hiyo inasema.
Ripoti hiyo ilipitishwa baada ya majadiliano ya kina yaliyodumu kwa wiki moja mjini Yokohama.
Kwa hisani ya BBC Swahili
No comments:
Post a Comment